Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Muheza kata gani maana nnashamba hapo lakini mvua hakuna
Wewe unalimia wapi mbona mvua zimenyesha na watu wameshapanda na waliopanda awamu ya kwanza sasa wanapalilia na waliopanda awamu ya pili mahindi yanaanza kuota
 
Kama unataka kwa ajili ya mahindi ya kuchoma kibiashara zaidi, panar 4m19 ni nzuri sana, mahindi yake matamu, angalizo ni kuwa yanaweza yakakomaa usifahamu ukasituka yamekwishaanza kukauka, kwani majani yake utakuta mabichi kumbe ndani yameanza kukauka.
 
Hebu tupe mrejesho maana haya mawazo yalikuwa ya mwaka 2010 sasa ni 2017 je kuna mafanikio ili na sisi tujiunge na wewe
 
Nice paper work, I wish all the best to be on that level
 
Hebu tupe mrejesho maana haya mawazo yalikuwa ya mwaka 2010 sasa ni 2017 je kuna mafanikio ili na sisi tujiunge na wewe
Mkuu na mm nalima na ni mwanafunzi chuo cha st.joseph nipo hapa nalima morogoro hekari mbili za mahindi na yamekua saivi kama vip karibuni mjinyakulie mashamba kwa hekari moja laki tano na jumla nimetumia laki tisa tu mpaka yalipofikia na pia kuna alizeti kwa hekari moja na jumla nimetumia 1.8 kwa hekari mbili pamoja na mahindi.
[emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116] [emoji116]
 
Hongera sana mkuu...Mungu aendelee kuwa nawe
 
Moro ipi yenye mashamba karibu na mto ili niweze kutumia pump za kumwagilia mkuu!
 
Moro ipi yenye mashamba karibu na mto ili niweze kutumis pump za kumwagilia mkuu!
Mkuu hapa sisi tunategemea mvua za mwenyezi mungu tu hamna kumwagilia hapa na sijawahi ona mtu anamwagilia shamba tangu nianze kulima hapa morogoro na ardhi yenyewe ina rutuba hamna haja na mbolea na kama kuna mtu yupo dar au moro na mikoa mingine na yupo interested kulima tunaweza kuchekiana kwa hizi namba hapa
0716-473786/0755-922096.
 
Ni hapa mikese mkuu hii sehemu yenye mizani ya kupimia uzito wa magari afu unaingia ndani kabisa penye mashamba kabla hujafika morogoro mjini karibu tupo.
 
Asante kwa tsarifa, tatizo la kusubiria msimu huwezi kufanya kilimo cha kibiashara, vipi ukichimba maji yanapatika kina kifupi?
 
Asante kwa tsarifa, tatizo la kusubiria msimu huwezi kufanya kilimo cha kibiashara, vipi ukichimba maji yanapatika kina kifupi?
Maji yapo ni wewe tu ukitaka uchimbe umwagilie is up to you ila kwa hizi mvua sidhan kama utadiliki kumwagilia shamba.
 
Habari wakuu, poleni na kazi!

Wakuu nataka kulima mahindi kwa njia ya umwagiliaji, yani nipande mwezi wa sita nikitarijia kuvuna mwezi wa 10.

Naombeni kuuliza kwa wazoefu, ambao wamewahi kulima kilimo hiki wakati huu wa kiangazi, je naweza kulima na nikapata faida ukizingatia na gharama za umwagiliaji?
Je mahindi hayatakuwa na matatizo yoyote ukizingatia sio msimu wake?

Asanteni natarajia kupata mawazo zaidi kutoka kwenu.
 
Safi sana hii kitu, ngoja nami nifuatilie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…