Nimeamua kuoa baa medi

Ina maana baamedi sio mwanamke?Ungekua umepata mmoja kati ya hao unaowaponda ungekuj kutuambia hapa?
 
mke mwema hutoka kwa Mungu!
Haijalishi anafanya kazi gani, mradi tabia iwe njema.
 
Acha unyanyasaji. Baamedi ni sawa na wanawakd wengine, ana tabia sawa na wanawake wengine. Ana uwezo sawa na wanawake wengine.

Napenda tu kukushauri uwe makini unapoamua kumchagua. Usimchague kutokana na kazi yake. Usije ukarudi jamvini tena na kuanza kulia.
 
Omba Mungu akupe mke mzuri, mambo ya kazi gani anafanya hayana maana sana. Kazi ni kazi tu alimradi ni ya halali.
 
ni mwanamke kama wanawake wengine mengine ni tabia ya mtu binafsi kila la heri
 
Mkuu isijekuwa ni wewe uliyevuta BAAMEDI, unataka kutushawishi na sisi tufuate mkumbo!
Acha bana Tunamshukuru Mola, wakwetu wametulia.
 
well said!
 
ni mwanamke kama wanawake wengine mengine ni tabia ya mtu binafsi kila la heri

Safi chauro. Lakini tafiti zinaonesha kuwa hawa wana nidhamu na huwa wanatulia sana katika ndoa tofauti na masistaduu ambao huwa wanapenda maisha ya juu hata kama hawana uwezo wa kufikia huko.
 
Mkuu isijekuwa ni wewe uliyevuta BAAMEDI, unataka kutushawishi na sisi tufuate mkumbo!
Acha bana Tunamshukuru Mola, wakwetu wametulia.

Hata kama hajatulia utajinadi hivyo tu... Unaye kwanzaa!?
 
Mke ni mke bila kujali kazi yake. Ila utakuwa tayari kuvumilia wateja wake wa zamani wakisalimia? Sikilza kwanza moyo wako unakutuma vipi

Kwani nimekwambia nitafungua baa home?
 
Kama umeamua kuoa mfanyakazi wa baa fanya hivyo wewe kama wewe.Sio eti kwa sababu fulani nae alifanya hivyo.Kwa kukusaida tu ni kwamba,mtu kufanya kazi baa sio kipimo cha uhovyo ama umalaya ama kutumika sana SI KWELI!Endelea na mchakato mkuu.Kama bahati iko upande wako basi utapata mke bora kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…