Niliwahi kutoa topic hapa kuwa "Sintopiga kura kwenye uchaguzi wa 2010", nilikuwa serious kabisa na uamuzi ule kwa wakati ule. Ila baada ya tafakari ya kina na kusoma makala mbalimbali pamoja na kufuatilia kwa umakini umuhimu wa kupiga katika kuchagua viongozi halali na makini nimeamua kupiga kura yangu. Pia kilichonisukuma kupiga kura yangu ni baada ya kugundua kuwa kuna maelfu ya Watanzania ambao hawatapiga kura kutokana na sababu kama zangu hapo awali au zaidi ya zile; kwa mfano wiki moja iliyopita niliongea na kijana mmoja na akasema hawezi kupiga kura kwasababu tayari MSHINDI ANAFAHAMIKA, sasa watu wa aina hii kama wako miatano kila wilaya ina maana kuna balaa kubwa sana na hii kupelekea kuwa faida kwa wagombea wasiokubalika!
NB:-Elimu ya uraia na ya kupiga kura bado inahitajika kama Tanzania inahitaji mabadiliko ya kweli kwenye uchaguzi wa viongozi na elimu hiyo ianzie vijijini kuja mijini tuache makelele tu kwa watu laki tano wakati watu milioni kumi na tano hawasikii hayo makelele.
Niko katika harakati za kuhakikisha kuwa Watanzania wengi zaidi wanapiga kura ila sintoharakatisha Mtanzania yeyote kumpigia mgombea au chama fulani kura yake maana hata kura yangu ni siri yangu kwa kiongozi makini