Nimeamua kurudi CCM rasmi

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Niliachana na ccm mwaka 1984 kwenye ile vita ya uhujumu uchumi iliyotumiwa vibaya na watendaji wa ccm chini ya hayati waziri mkuu Edward Moringe Sokoine...!!!!
Biashara za familia zilizikwa na ile vita kwa uonevu mkubwa sana...kuingia 1985 ya mzee ruksa sikuwa na hata chembe ya kuwa ccm
Mzee ruksa Alivurunda zaidi aliporuhusu biashara huria bila ya maandalizi na kwa mara ya kwanza wabongo tukaanza kuendesha magari reject toka Japan maarufu kama JABA....Na ndio tukabadili mfumo wa plate number kutoka TZ na zile plate number kwa mikoa yaani AR-Arusha, TA-Tanga nk na kungia kwenye mfumo wa TZA, TZB, TZC ... ..Mfumo ulioua registration za mikoa
Tukawa sasa tuna sajili plate number mpya gari mtumba reject.PATHETIC POOR PEOPLE...!!!! Peugeot house ikafa rasmi

Akaja Ben Mkapa msomi nguli RIP ...Akafanya ubinafsishaji mkubwa sana...chote alichokijenga Mchonga kwa miaka 37...CCM ya Mkapa ikakifisadi overnight!!!!
National battery
Ubungo spinning
General tyre
Mang'ula tools
Ufi
National milling
RTC
TTCL
nknknk
Kilichomuumiza Mchonga kuliko vyote ni NBC ..kuuziwa makaburu kwa bei ya kutupa
Chuki yangu kwa ccm ikazidi..Hizi ndio zile nyakati kukawa na pengo la wazi kati ya walio nacho na wasio nacho..ikawa ukiwa na bendera ya ccm kwenye gari lako wewe ni untouchable...na ndio hapa Sumaye akiwa waziri mkuu akatangaza wazi kuwa UKITAKA MAMBO YAKO YAKUNYOOKEE KUWA CCM
Nyakati ni kurasa ...ukurasa wa Ben ukapita na makandokando yake yote..Akaja mzee wa msoga...wote hawa ni ccm ...yani wananchi tunapigwa mtungo bila huruma na watu walewale
Mzee wa Msoga..akalegeza kidogo..halafu akalegeza kabisa...kama taifa tukaingia kwenye auto mode...yaani tulikuwa tunaenda tu
Baada ya msoga tukapaa mpaka Chuttle tulikofungua kurasa mpya baada ya kufunga za Msoga...
Ni wazi kurasa za chuttle ndio zitahimitisha kitabu kikubwa cha zama za ccm...yaani TUNASOMA UKURASA WA MWISHO KISHA TUSOME NENO TAMATI tufunge rasmi kitabu cha ccm tukakiweke maktaba kama kumbukumbu

Sasa kwanini nataka nirudi kuwa sehemu ya kitu kinachofikia kikomo?
Nataka niwe mtunza kumbukumbu...kitabu KIPYA kijacho kinaweza kukitupa ghalani kitabu cha zamani..ghalani kuna vumbi na tandabui ..nataka niwe mfagizi ghalani


Ni hulka yetu kutunza wazee waliomaliza muda wao..nataka nirudi nyumbani ccm nikamtuze mzee wangu huyu...nataka nikae naye kwa upendo huku nikimkumbusha madhila yote ubabe wote ukatili wote mabaya yote aliyotufanyia katika maisha yake yote ya miaka 59...

Tangu leo kwa akili zangu na bila kushurutishwa na ahadi nono za kitapeli za kuunga juhudi NATANGAZA RASMI KURUDI CCM ...Lumumba nipokeeni...nimeshazoea kuwa MPINZANI
 
Mkuu Mimi mwanafasihi nimekuelewa kifupi wanyakyusa sehemu za makaburini wanaziita masyeto naona unarudi kutunza masyeto kikoree .

Sisi mamong'oo ngoja tuende kanani.
Bila kuyatunza makaburi kuna mengi yanaweza kufanyiwa
Wanga watayageuza vilinge
Wachawi watayageuze machimbo ya malighafi
Vibaka watayageuza maficho na ukabaji
Wahuni watayageuza vijiwe vya bangi na ubakaji
Machangu watayageuza gesti bubu
 
Bila kuyatunza makaburi kuna mengi yanaweza kufanyiwa
Wanga watayageuza vilinge
Wachawi watayageuze machimbo ya malighafi
Vibaka watayageuza maficho na ukabaji
Wahuni watayageuza vijiwe vya bangi na ubakaji
Machangu watayageuza gesti bubu
Basi sawa mkuu hongera kwa kwenda kuishi makumbusho japo mamong'oo watakuona unaenda antklokwais ......!!! Usijali
 
Ni kweli chichim itakuwa mpinzani hivi punde
Kurasa 27 za mchonga ndio pekee zilikuwa na maono na miongozo iliyonyooka..kurasa zingine zote zilizofuatia zilikuwa kama sio kuku wa kideri basi kuku wa mganga...anachinjwa halafu anaachwa arukeruke hadi kifo
Na kuna kurasa zilikuwa kama BISI KIKAANGONI[emoji2957][emoji1550]
 
Uongozi wetu na hatma ya Tanzania kilinunuliwa na tiss chote Sasa wakakinunue na kile cha amstadam mpaka kule Amazon. Mwaka huu tunawapiga kila sehemu mkiiba kura hatukubali mkipiga watu risasi the Hague weweeeeeeeeee
 
Uongozi wetu na hatma ya Tanzania kilinunuliwa na tiss chote Sasa wakakinunue na kile cha amstadam mpaka kule Amazon. Mwaka huu tunawapiga kila sehemu mkiiba kura hatukubali mkipiga watu risasi the Hague weweeeeeeeeee
Na cha TUJIKOSOE also by Mwal. J.K Nyerere
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…