Nimeamua kusaidia Mtu mwenye wazo la biashara bora - Fremu ya Biashara Sinza

safi sana mkubwa, hii ndio nataka kuona hapa. Mm kama ungekua unapangisha fremu, wazo langu na mtaji wangu ungenipata.
Zoezi letu lilifungwa Tarehe 1, October 2022.

Tumetumia siku 3 kuipitia mawazo 35 yaliyo wasilisha DM na memgine matatu(3) ya hapa kwenye comment, jumla tulikuwa na mawazo 38,

Mawazo yaliyo fanikiwa kuingia 10bora ni:

1. Wazo la Nafaka (Wamefungana wapo wa5 walio wasilisha wazo hili.)

2. Wazo la Mayai ya Jumla.

3. Wazo la Nguo

4. Wazo la Butcher

5.Wazo la Ufundi Simu na uuzaji wa Accesory za computer na simu.

6. Wazo la Stationary n Uduma za Miamala

7. Wazo la Juice ya Miwa na Mtindi.

8. Wazo la Car lubricate and Accesories.

9. Wazo la Kuuza Movies za Soft copy na Accesories za computer

10. Wazo la Supu za Ulimi, Kongoro na Kuku.


Tunapitia mawazo haya 10. kwa ufainisi kuona walio wasilisha kama wame weza kuelezea na kuchaganua vyema proposal zao.

Mshindi ata tangazwa hapa kati ya leo na kesho.

Vitu vinavyo zingatiwa ni :

1. Mleta wazo ameweza kuelezea mtaji husika ulio tajwa? kama amevuka ukomo wa mtaji anasemaje ana uwezo wa kujazia au vip?

2. Je amefafanua mchanganuo wa wazo lake kwanzia Bei ya Manunuzi na ya Mauzo?, ameweza kuonyesha faida itakavyopatikana?, ame weza kuelezea matumizi ya mzunguko mzima wa biashara mpaka kuifikia faida?

Je wazo lake ni halisia au haliendani na uhalisia wa kibiashara (Hivi haelezi yeye ila.mm na mtaalamu wa biashara tunavitafakari kwenye wazo lake)

Je faida anyo izungumzia inaweza kweli kumpa chakula cha kila siku na akansave kukuza biashara au ndio mtaji utaliwa chakula,

Je faida anayo izungumzia ina fikia viwango vya faida ya kujiendesha kibiashara au ndio risk ya mtaji mkubwa alfu faida haifiki hata asilima 5% maana biashara yenye tija faida inatakaia iwe 12%, 15% au hata 20%

Tukijiridhisha tuta mtangaza mshindi ndani ya siku mbili na ataitwa Dm atoe number zake tumpigie na akikabidhiwa mtaji na frame apige picha na tutamtaka aje kutoa ushaidi hapa ili watu wajue fursa inachangamkiwa n wale wasio penda kuamini wawe na imani
 
MSHINDI WETU:

Ningependa kumtangaza Mshindi ambaye kikukweli aliweza kwenda zaidi ya mategemeo yetu ya uwasilishaji wazo lake.

Kwanza kabisa, kaweza kuchanganua kuanzia Atakavyo anza biashara kwa kuulinda mtaji, kaweza kuonyesha Matumizi ya kila siku kuanzia Umeme nauli yake, kaonyesha mzunguko wa gharama zote kuanzia kuagiza bidhaa mpaka kumfikia eneo lake, Mbinu za kuwapata wateja, kaonyesha kila akiuza faida inapatikana asilimia ngapi, na ameweza kuivunja kwa siku kwa week na kwa mwezi, mpaka kwa mwaka, mpaka ameweza kuonyesha akitanuka kibiashara atakavyo ongeza kijana wakumsaidia na atakavyo mlipa.

Kwa kweli huyu alitulia sana kuandaa wazo lake kwa uhalisia kabisa, tofauti na wengi walitaja wazo tu na walio jitaidi kuelezea mawazo yao hawakuweza kufafanua matumizi ya biashara, hawakuweza kuonyesha mbinu za watakavyo tafuta wateja, wala mstakabali wa ukuaji wa biashara itakavyo kuwa ndani ya mwaka kwa kuonyesha mzunguko wa siku , week , mwezi mpaka mwaka.

Niseme tu huyu jamaa kama ana shinda basi ni uwezo wake wakujieleza na kuto kuficha taarifa yoyote kiasi cha kumfanya mtoa mtaji na frame kufikiria kama kweli atafanya hivi alivyo andika niwazi anastahili kuaminika n kuongezewa hata mtaji uko baadaye nili kuwe n branches na management iwe chini yake.

Mabibi na mabwana naomba nimtangaze Mtu anaye jiita WatesiWETU ambaye aliwakilisha wazo la "NAFAKA" kama nilivyo sema wazo hili liligusiwa na watu watano.. lakini kwajinsi alivyo liwakilisha huyu alikuwa na upekee sana na hakuacha shaka ya maelezo.. alikuwa deep na alifanya research ya bei za nafaka za aina 12 na maeneo zinapopatikana na mpaka suppliers watakavyo mfikishia mzigo, alieleza bei ya uzani ule mkubwa wakupimia mazao, na uzani mdogo wa kupimia wateja wanaochukua kilo chini ya 5, hadi mifuko ya kuweka dukani atakapo ipata karikooo atakuwa akiwauzia wateja watakao kuja bila mifuko na hii nibiashra within the business, pia alielezea mafuta yakula ataanzaje kuchanganya dukani.

TUNA MUOMBA HUYU MTU ANAYE JIITA WatesiWETU AJE DM ATUPE NAMBA YA SIMU TUWASILIANE JINSI YA KUKUTANA NA PIA ATOE RUHUSA KAMA ATA TURUHUSU TUPOST ANDIKO LAKE WATU WAJIFUNZE. MBINU ZA KUANDIKA MCHANGANUO NA WATAKAO LIPENDA WALITEKELEZE WAZO HILO POPOTE WALIPO.
 
Wazo zuri sana hili maana huku kuna wateja kama wote aise.
 
Rahisi tu sema una milion2 unahitaji wazo la biashara , sio kuzunguka Mara unasafiri, utashare mtaji hizo zote ni kelele , nenda direct una mtaj lakin hujui uweke kwenye biashara ipi , wadau watakusaidia
 
Tunaomba hilo wazo public.
 
Asantee sanaaaa..
Aminaaa ndugu.
 
Ucjali.. Utaratibu wangu wa Masha Fungu la 10 Huwa natoa kwa watu.. kama shukrani kwa Mungu... hichi nilicho toa kwa WatesiWETU ni sehemu hiyo kwa kipindi cha mwezi wa 6-9.. hivyo kwa kipindi kijacho cha 10-12 kutakuwa na shukrani kwa mtu mwingine na itategemea na mapato ya kipind husika.. huwenda ikwa zaidi ya hii ya sasa. hivyo linda wazo lako ukiwa tayari uta lileta dm litafakariwe.
 
Tutumie huo mchanganuo tujifunze
 
Kwahiyo hakukupa ruhusa ya kulishusha hapa? From above it looks very interesting jinsi ulivyomuelezea mshindi na briefing ulizotupa. Kama kakupa ruhusa shusha nondo jinsi alivyo kuconvince detail-wise
 
Asantee sanaaaa..
Aminaaa ndugu.

Hongera. MRUHUSU ASHUSHE NONDO ZAKO KULE DM kama alivyosema. Should you be fearful kuhusu waigaji... You know what they may copy you, but bound to fail because lacks your intellect and spirit ila ata wakiku-outperform you should be proud for your kindness and selflessness
 
Mkuu Hell2Heaven ,
If its true, you have an impeccable characteristing... Holy Tithing like this one will give you a wonderful return.

Basi share best presentation hiyo. And hao wanao jibrag kwamba wana best idea wafanyie namna wapresent kuprove
 
Watu wengi huanzisha biashara lakini hazidumu kwa sababu kadha wa kadha!

Tunaomba presentation ilivyo itusaidie kuboresha biashara zetu zinazofanana na hiyo, ahasante! Hell2Heaven
 
Mungu azidishe pale ulipo toa akuongezee amen [emoji120].
Piga kazi watesiwetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…