Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
katika harakati zangu za kuwa na sampuli mbalimbali; wenye chura matata, warefu, wafupi, wembamba, wanene n.k, nimeona hayo maisha ni ubatili mtupu.
Mwisho wa siku wanakuwa hawana shukrani, zaidi ya kuwa wapigaji tu; wengi wanaingia kwenye uhusiano kama ajira.
Utasikia bebii nimeishiwa hiki, mara mtoto amemeza mtungi wa gesi, mara natakiwa saluni n.k.
Kwa ujumla, walikuwa wananifanya kichwa kuchanganya mafaili na moyo kwenda mbio.
Kwa sasa nimeamua kubaki njia kuu nile mafao yangu ya uzeeni na mke wangu; waswahili wanasema, uliyeokota naye kuni ndio utakayeota naye moto.
Kwa michepuko tuliozaa pamoja, tuonane baada ya miaka 20 katika kuwaozesha hao watoto wetu; msisahau kuniletea kadi; hakutakuwa na kupasha kiporo.
Kijiti namkabizi kijana mmoja machachari hapa jukwaani, ikiwezekana mpendekezeni.
Mstaafu baharia,