Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu nimeamua kuwa cheater, uzoefu wangu kwenye maswala ya mahusiano umekuwa sio mzuri japo nilijitahidi kuwa mwaminifu sana. Kuwa single siwezi , solution ninayoiona ni kutokuwa serious kwenye mahusiano na kudanganya kama ambavyo wengi wamekuwa wakidanganya. This world is not fair kabisaaaaa, unachotenda sicho unacholipwa. Ninajua kuwa cheater sio vizuri lakini nifanye nini wakati dunia sio fair?? niwe natenda wema alafu malipo kwa Mungu hadi lini?? Dunia ya leo kila kitu kinapelekwa kisanii hivyo na mimi nimeamua niishi kisanii kuanzia mwaka 2012.
Sio sahihi kabisa dada yangu kwa maamuzi unayotaka kufanya!Lakini elewa mambo haya yanatokea kwa sababu ya
Kukosa kujua neno la Mungu linasema nini juu ya zinaa katika marefu na mapana yake, kumewafanya watu wengi wanaswe na mtego huu mbaya.Watu wa Mungu wengi sana nyakati hizi wanaangamizwa kwa kukosa maarifa maarifa juu ya mapenzi ya Mungu. Na eneo mojawapo ambalo linaangamiza wengi ni eneo la uzinzi.Hosea 4:6 (Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa
..)
ushauri mzuri wa biblia utakaoweza kukusaidia kuishinda dhambi hii ya zinaa.
1. DUMU KATIKA MAOMBI
Yesu pale Gethsemane alisema;
Je! Hamkuweza kukesha pamojanami hata saa moja? Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi. Lakini mwili ni dhaifu (Mathayo 26:40-41)
Ukisha mpokea Kristo moyoni mwako, roho yako inakuwa radhi kumtii Kristo na kutokutenda dhambi; lakini kumbuka kuwa roho yako bado imo katika mwili ulio dhaifu ambao unataka kutenda dhambi.
Yesu Kristo alipokuwa akifundisha kuomba alisema sehemu mojawapo ya maombi yetu iwe;
Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu, Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu na utukufu, hata milele, Amina. (Mathayo 6:13). Watu wengine huwa wanaisema sala hii kikasuku bila kuangalia uzito wa maneno yaliyomo. Lakini ukijua uzito wake hutachoka kuomba kwa
Na usitutie majaribuni. Jaribu mojawapo ambalo unapaswa uombe uepushwe nalo ni zinaa.
Wengine wakianguka katika zinaa, utawasikia wakijitetea na kusema;
Nilibanwa mno hata nikashindwa kujizuia nikaanguka katika zinaa.
Unaweza ukajitetea hivyo, lakini ungeamua kushinda, Bwana angeuwezesha kushinda. Kwa kuwa imeandikwa;
Ninyi watoto wadogo mwatokana na Mung; nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye NDANI YENU NI MKUU KULIKO aliye katika dunia. (1 Yohana 4:4)
Lakini katika mambo hayo yote TUNASHINDA NA ZAIDI YA KUSHINDANA kwa yeye (Yesu Kristo) aliyetupenda (Warumi 8:73)
Na ni budi pia ukumbuke, kila jaribu lina njia ya kutokea, si katika njia ya kushindwa bali katika mlango wa ushindi.
Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke. Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu, ila Mungu ni mwaminifu, ambaye HATAWAACHA MJARIBIWE KUPITA MWEZAVYO; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili. (1 Wakorintho 10:12-13)
Je! Hili si jambo zuri kufahamu ya kuwa Mungu wetu tunayemwabudu na kumtumikia katika Kristo ni MWAMINIFU? Hili ni zuri sana! Kwa kuwa hatatuacha tujaribiwe kupita tuwezavyo, lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili tuweze kufanya nini? Ili tuweze KUSTAHIMILI! Jina la Bwana libarikiwe daima!
Tafsiri nyingine inasema
Anayedhani amesimama imara ajihadhari asianguke. Majaribu mliyokwisha pata ni kawaida kwa binadamu. Mungu ni mwaminifu. Naye hataruhusu mjaribiwe kupita nguvu zenu, ila pamoja na majaribu, yeye atawapeni pia nguvu ya kustahimili na njia ya kutoka humo salama.
2.IKIMBIE ZINAA.
IKIMBIENI ZINAA. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. (1 Wakorintho 6:18)
Ni kweli ya kwamba, biblia inasema
Basi mtiini Mungu. Mpingeni shetani, naye atawakimbia.(Yakobo 4:7). Lakini biblia haisemi ipingeni zinaa, bali inasema IKIMBIENI ZINAA!
Watu wengi wameanguka katika zinaa, kwa kuwa wanajaribu kupingana nayo. Mwisho wake wanazidiwa na wanazini. Kwa nini hawafuati ushauri huu wa biblia unaosema ikiembieni zinaa?
Katika kitabu cha Mwanzo 39:6-12 tunasoma habari za Yusufu jinsi alivyokabiliwa na jaribu la uzinzi, na jinsi alivyopona kwa kukimbia!