Nimeanzisha biashara Kariakoo, inasuasua nifanyeje iweze kuwa kwenye hali nzuri

Harry Barry

Member
Joined
May 12, 2016
Posts
14
Reaction score
16
Wanandugu msaada tafadhali.

Ninafanya biashara Kariakoo duka la nguo za kiume na nimewekeza pesa nyingi Ila mambo hayaendi kabisa tatizo limeanza baada ya Corona maana nimeanza biashara mwezi wa 1 Corona ikaja kuharibu Kila kitu.

Msaada nifanye Nini ili nipambanie biashara yangu iweze kuwa katika Hali nzuri.

N.B: Napokea maoni hasi na chanya pia.
 
Boss kwanza hongeraaa...
Kua na fremu k.koo sio Mchezo...

Ni biashara yoyote inayoanza boss inachuku mda kuchangamka, kipindi ulichoanza kama ulivyosema, Ushindani uliopo n.k.

Mi nakushauri komaa, japo ungeomba ushauri kabla ningekushauri ufungue hilo duka mtaaani au sehemu nyingine kama mwenge n.k

Lakini hamna kilichoharibika, pambanaa, utatoboa.
Unauza jumla na reja reja au?, Naweza siku moja kuja kukuunga mzigo wa jumla.
 
Nakazia
 
Kwenye biashara kuna kipindi cha mpito...wengine wanasema ni miezi 18!(which is true)

Kwasababu gan? Mwaka una miezi 12....na miez inayobakia kufunga 18mths ni 6! Kwahyo utajua wewe ni season gan biashara inaraise ..! Measn ukianza season ya miez, 6 unajua kabisa kipindi cha 12moths biashara ilishow namna hii na hii.so unajua kbs hii ni kawaida kuuza au kutouza...( sijui kama umeelewa)

Kwahyo hapo wewe acha kupanic..hapo biashara yako inajitengeneza yenyewe then itakuna kusimama poa..yaan utakuja fahamu kutoka june had sept hakuna biashara..kutoka oct had dec kuna biashara...!upo kwenye mpito huo.

Wengine wataalam wanadai biashara kusimama ni siku 999!(haka ni kakanuni )..means miaka 3 na miez kadhaan.ukitusua hapo hata aje mchawi wewe hutikisiki...nenda na hizo formulas.
 
Jaribu kuongeza huduma ya home delivery.

Nunua ads za mitandao ya kijamii kuongeza idadi ya wateja nje ya wale wanaokuja k/koo hata jf pia itumie weka mpaka kwenye e-commerce kama kupatana, zoomtanzania, jiji nk
 
Nataka kujua mtaji wako na kiasi gani in jumla au rejareja?
 
Yah nauza jumla na rejareja
Ila mkuu unadhani nifanye kitu gani ama niongeze nini ili graph yangu ya biashara iweze kwenda vizuri???
 
Nataka kujua mtaji wako na kiasi gani in jumla au rejareja?
Yani mkuu kujua mtaji wa mtu kwenye biashara yake unamuamuru NATAKA, Seriously?

Kuna vitu ni siri ya mtu inabidi uombe na ana uhuru wa kujibu au laaa..
Labda hapo kwenye kujua ni jumla au reja reja.

Nimtazamo tuu boss.
Niwie radhi kama nitakua nimekukwaza.
 
Yah nauza jumla na rejareja
Ila mkuu unadhani nifanye kitu gani ama niongeze nini ili graph yangu ya biashara iweze kwenda vizuri???
Upo mtaa gani boss?
 
Shukrani mkuu hapo nimekuelewa
 
Jaribu kuongeza huduma ya home delivery.

Nunua ads za mitandao ya kijamii kuongeza idadi ya wateja nje ya wale wanaokuja k/koo hata jf pia itumie weka mpaka kwenye e-commerce kama kupatana, zoomtanzania, jiji nk
Shukrani sana
 
Yani mkuu kujua mtaji wa mtu kwenye biashara yake unamuamuru NATAKA, Seriously?

Kuna vitu ni siri ya mtu inabidi uombe na ana uhuru wa kujibu au laaa..
Labda hapo kwenye kujua ni jumla au reja reja.

Niwie radhi kama nitakua nimekukwaza.
Sorry mkuu nimetumia neno nataka ila sikuwa na nia mbaya ya kuku command ni kwamba huwezi mshauri mtu kuhusu biashara pasipo kuijua vizuri hiyo biashara usiwe na hofu we kuwa wazi me sikujui na hunijui ni vile umeomba ushauri nikaone nijue baadhi ya vitu kabla ya kukushauri.
 
Boss Mhusika sio mimi...
Ulikua ni mtizamo tuu, usijali tupo pamoja.
 
Jaribu kuongeza huduma ya home delivery.

Nunua ads za mitandao ya kijamii kuongeza idadi ya wateja nje ya wale wanaokuja k/koo hata jf pia itumie weka mpaka kwenye e-commerce kama kupatana, zoomtanzania, jiji nk
Ariri huu ushauri juu ukiufanyia kazi utakusaidia kwa kiasi chake, pia jaribu kutumia na machinga wakuuzie mzigo wenye maduka wengi kko wanafanya hivyo.

Mwisho kabisa wafanyabiashara wengi wanalalamika biashara haziendi kaugonjwa kameleta balaa.
 
Yah nauza jumla na rejareja
Ila mkuu unadhani nifanye kitu gani ama niongeze nini ili graph yangu ya biashara iweze kwenda vizuri???
Nunua ads za mtandao hasa facebook na instagram nakuambia utapokea watejana order toka mpaka mikoani na haitakucost sana online campaign hata elf hamsini inatosha kwa kampeni ya week lakini matokeo yake ni makubwaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…