Nimeaza kuandika vitabu, Nahitaji msaada zaidi

Ahmed Saidi

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2019
Posts
1,588
Reaction score
3,487
Salamu wapendwa

Katika kitu ambacho nilikuwa natamani basi ni kuwa na kitabu changu (Ni passion yangu). Nime-plan kuandika vitabu kadhaa Kama reference kwa wanafunzi.
Basi Kwenye hii likizo nilianza kuandika kitabu kimoja, ni ngumu lakini naona inawezekana.

Nimepanga kuandika vitabu sita panapo majaaliwa. Ingawa vitabu hivyo ni too general (havita fuata mtaala) lakini naamini vitawasadia wanafunzi kujifunza kwani materials yake yatakuwa ni zaidi ya mtaala wa somo husika.

Nimepanga kuandika vitabu vifuatavyo;
1. Kitabu cha Geomorphology, (Infact hiki ndio nimeanza nacho na sasa nipo kama page ya 50)
2. Climatology
3. Soil Science
4. Practical Geography
5. Human Geography
6. General Psychology (hiki ni kwa ajiri ya jamii kwa ujumla, hakiwalengi sana wanafunzi ingawa nao wanaweza kukitumia kama reference).

Katika vitabu hivi nitafanya yafuatayo;
-Nataka kutumia picha, michoro na mifano halisi ili kuwasaidia wanafunzi kuelewa.
-Lugha rahisi, tables na summarization.
-Wide coverage (yaani nitagusa kila aspect ya topic fulani).
-N.k.

Najua kuna changamoto katika kutimiza wazo langu hili, ndio maana nimeleta uzi huu. Hivyo naomba wadau wazoefu, waandishi nguli na wachapishaji wa humu JF wanijuze kuhusu mambo ya msingi ya kufanya kutimiza ndoto yangu hii.

Shukrani.
 
Hongera mkuu.....endelea kupambana....tunapenda ulete rivarly competition kwa kina msabila vs zisti kamili[emoji23][emoji23]
 
Kuna rafiki yangu tumemaliza nae chuo mwaka huu, alizindua kitabu chake japo sio academic book, ni Cha social lakini nahisi anaweza kukupa experience kidogo, namba zake hizo
Shukrani sana Kaka, Mungu akubariki
 
Wakuu nilichukua result slip ya forms six ila Vijana wa bodaboda wamepita na mkoba result ikiwa ndani naomba msaada kwa anaejua nianzie wapi
 
Umefikia wapi,tupe mrejesho
Nashukuru sana ufuatiliaji wako,

Mpaka sasa nimekamilisha vitabu viwili ambavyo ni Geomorphology na Climatology. Sasa nimeanza cha Practical Geography, then nije Soil Science na hatimae nimalizie Human Geography.
Naenda taratibu Kwa sababu kuandaa vitabu inahitaji utulivu na umakini ili kupata kitu kilicho bora
 
Wakuu nilichukua result slip ya forms six ila Vijana wa bodaboda wamepita na mkoba result ikiwa ndani naomba msaada kwa anaejua nianzie wapi

Karipoti polisi kisha nenda nacte uanze process za kutengenezewa nyingine.
 

Bless. Tunaweza kuvipataje hivyo vilivyo tayari.
 
Hizo phamlets hapo juu zipo tayari, nimeprint kama pamphlet kwasababu sijapata sehemu nzuri ya kuprint kama kitabu. Ukihitaji nicheck Kwa 0728367208,
Niko Mbeya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…