Maseto
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 944
- 545
Janja ya kushinda kesi kwa wakili huyu ambaye pia huiwakilisha ccm kwa baadhi ya kesi ni uandaaji wa mashtaka.huwa anahakikisha mashtka yanatengenezwa kwa namna ambayo itamsaidia ashinde kesi.mfano ni ile kesi ya zombe.kesi ilikuwa na mashtaka ambayo hata mtu asiye mwanasheria angejua zombe atashinda.mfano wa pili ni ile kesi ya ghorofa lililoanguka hivi karibuni pale kisutu.watuhumiwa wote 11 wametuhumiwa kwa kosa la aina moja-kuua bila kukusudia.tatizo la watanzania huwa tunapiga tu mayowe na kuridhika tu na wakosaji kupelekwa tu mahakamani bila kujali mwendesha mashtaka kaandika nini.kwa hiyo, hiyo kesi ya ghorofa watuhumiwa wamekwishashinda kabla haijaanza.