Nimebaini janja ya wakili msemwa kushinda kesi anazosimamia

Maseto

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
944
Reaction score
545
Janja ya kushinda kesi kwa wakili huyu ambaye pia huiwakilisha ccm kwa baadhi ya kesi ni uandaaji wa mashtaka.huwa anahakikisha mashtka yanatengenezwa kwa namna ambayo itamsaidia ashinde kesi.mfano ni ile kesi ya zombe.kesi ilikuwa na mashtaka ambayo hata mtu asiye mwanasheria angejua zombe atashinda.mfano wa pili ni ile kesi ya ghorofa lililoanguka hivi karibuni pale kisutu.watuhumiwa wote 11 wametuhumiwa kwa kosa la aina moja-kuua bila kukusudia.tatizo la watanzania huwa tunapiga tu mayowe na kuridhika tu na wakosaji kupelekwa tu mahakamani bila kujali mwendesha mashtaka kaandika nini.kwa hiyo, hiyo kesi ya ghorofa watuhumiwa wamekwishashinda kabla haijaanza.
 

Kwa hiyo tuseme huwa anakuwa na ''mawasiliano maalumu'' na mwendesha mashtaka ya kumfanya aandae mashtaka fyongo ambayo wanajua lazima mshtakiwa atashinda? Huu mtindo upo hasa kama mshtakiwa ni tajiri mwenye fedha nyingi, anaambiwa atoe fedha ya maana ambayo wakili na mwendesha mshtaka watagawana!
 
Acha ubwege, hiyo si ndiyo kazi ya wakili! Vinginevyo hakuna haja ya kuwepo
 
Acha ubwege, hiyo si ndiyo kazi ya wakili! Vinginevyo hakuna haja ya kuwepo

Kazi ya wakili kushirikiana na mwendesha mashtaka, kuandaa mashtaka fyongo ili mtuhumiwa ashinde kesi???
 
Ni kesi gani inayohusu/ gusa kitu cha sisiem ishawahi kuhukumiwa accordingly? Zombe alishinda, Balali kafa bila kuonyeshwa hata picha wala ndugu kushiriki msiba, Epa wezi wanarudisha fedha bila kutajwa wala kushitakiwa, Watorosha tembo hakuna anaeshitakiwa, Nyamongo wananchi wanakufa kwa maji ya sumu - hakuna kesi na uchunguzi miaka kibao majibu ziro, Kamanda wa polisi anauwa kadamnasi - hakuna kesi, Dowans - kamua wavuja jasho lipa deni, Madawa bandia na bidhaa zingine - hakuna kesi, na zinginezo kibao huku ngazi za chini. Kesi zote huishia kwa makatibu wa chama na mwenyekiti au mwendo wa tume tu Refer. Mkoa wa Rukwa, Bukoba etc.
Hakuna sheria ya wote nchi hii, kuna sheria kwa waiba kuku tu.
 
Acha ubwege, hiyo si ndiyo kazi ya wakili! Vinginevyo hakuna haja ya kuwepo
----- ni wewe usiyejua/kujifanya kutojua RUSHWA ilivyoshamiri katika mahakama zetu. Kwa nchi nyingi prosecutor anapanda cheo kutokana na % of conviction, hivyo wapo very careful na mashitaka wanayofungua. TAKUKURU wana zero conviction, je inaingia akilini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…