sasa wewe wa pm unataka malipo ya ziada?
Kwanini usiwe muwazi kwa kuweka mawazo yako hapa tuyapime?
Unataka uandikiwe pm ilimawazoyako yaonekane yameenda shule kumbe ukiyaweka wazi yatakua ya kitoto.
Usitumie advantage ya watu wenye shida kuwalisha mawazo ambayo hayajachujwa.
1.maisha siku zote yana changamoto.
2.changamoto zisikukatishe tamaa bali kukupa ari ya kusonga mbele.
3.nenda chuo cha uhasibu kurasini,mwone mkuu wa idara ya procurement mama mavis ni mtu mzima.utatoka unachekelea.
nawaunga mkono wote waliotoa maoni yao,
wasiwasi wangu ni kwa SAWEBOY anaficha nn wkt hili jukwaa letu ni la uwazi na ukweli.
Awe mwazi ili wengine nao wafaidike.Mnunu usikate tamaa bado una nafasi nzuri ya kusoma
nakupa mfano wa Hosea wa PCCB alikuwa karani wa mahakama
then akajiendeleza akawa hakimu ngazi ya mwanzo ,
hakimu mkazi na usisahau ni dr kabisa.songa mbele.
Nakupongeza kwa ujasiri wako wa kuweka wazi malengo yako yatatimia
na ukweli wako umekuweka huru.
Pole sana ndugu
usikate tamaa yote maisha
wasiliana na saweboy akupatie njia mbadala
pamoja na michango mingine ya wadau
Mungu awe pamoja nawe
ninaamini siku moja utafika pale unapohitaji kuwa
Pole sana NNUU!
Huna ya kukata tamaa kiasi hicho, sidhani kama kufeli kwako masomo ndiko kufeli maisha, ninachoamini maisha yataendelea na madamu maisha yanaendelea u can try again and again ukiamini kuwa kwa juhudi ufanyazo mwisho wa siku utafikia lengo lako.
Kuhusu CBE jaribu kupata ushauri kutoka kwao nafikiri itakuwa ni njia nzuri ya kuwa sure na kuokoa muda pia!!
Pole sana huna haja ya kukata tamaa na kupoteza matumaini kiasi hicho!!!!
Mungu akutangulie usifikie maamuzi ya kuutesa Moyo wako!!!
asante ila,
kinaitwaje?
Nakushauri jaribu kuöana nao moja kwa moja,alafu uone wanasemaje,na usiende chuo kimoja jaribu vngi,na ukienda urudi kutuletea riport.
NAHISI DUNIA IMENIGEUKA,
muda wangu wote,juhudi zangu zote,ndoto zangu zote,
maisha yangu yote naona kama ndiyo yamefikia mwisho.
Nilifanya mtihani wa kidato cha sita kama private candidates,
lakin NIMEFELI nina Dvn four (4) ya 18,GS-s,hst f, kisw -D,na eng f.
ndoto za kwenda chuo kikuu zimeyeyuka ghafla,
naona giza totolo mbele yangu,ila naamini kupitia,
hapa JF naamini wadogo zangu,wanangu,wajukuu zangu,
pamoja na wakubwa wenzangu mtanisaidia kimawazo nini cha kufanya.
mimi napenda sana nikasomee CBE mambo procurement kwa kuanzia na
diploma je ntaweza kufanikiwa kupata nafasi.Form nimeshachukua ila
sijarudisha,wasiwasi wangu je nitaweza kupata nafasi??.
matokeo ya form four yana hst-c,kiswa-c,eng-b,geo-d,
civic-d,. Yataweza kunisaidia kuingia diploma??.
Sitaki mkopo najilipia mwenyewe kwa sababu mimi siyo mwajiriwa,
nimejiajili mwenyewe na vibiashara vyangu vyenye uwezo wa kuniwezesha,
kumudu gharama zote kipindi chote cha masomo.
Sijapeleka jukwaa la elimu kwa sababu kule kuna wachangiaji wachache,
tofauti na huku ambako naamini nitapata mawazo mengi sana na yenye kunifaa.
Nawaomba muwe wa wazi tu,kama inawezekana sawa na kama haiwezekani niambieni pia. Ukweli wako ndiyo mafanikio yangu.
Samahani kwa maelezo marefu.
[/B]
Kaka jambazi ASANTE sana kwa mawazo yako,
hapo kwenye kukolezwa rangi napo pana maana sana tena sana,
ndiyo Tanzania yetu hii kila kitu watu wanageuza dili.
Lakin ningekuwa najua jinsi ya kuanza PM ningempm ili nimsikilize ushauri wake,
labda unaweza kunisaidia japo angeweka hapa labda ungeweza kuwasaidia wengi,
labda kuna wengine wenye tatizo kama langu japo hawajaweka wazi.
Mimi nimesoma CBE, najua pale kuna full time na night college;
hiyo fomu uliyochukua ni full time au night college? kwa appy in both full time & night college ili ukikosa full time uwezi kukosa night college