Nimechoka kuhama hama...

Rabama

Member
Joined
Dec 19, 2019
Posts
89
Reaction score
62
Mie ni mfanyakazi katika Company X Kutokana na kuhamishwa mikoa mbalix2 ki kazi...

Kwa sasa naitaji kusettle Sehemu Moja na familia yangu.

Wakuu naomba ushauri wenu

Kati ya Dar(nina nyumba), Iringa nina kiwanja, Mwanza (nina kiwanja), na Tanga...

Wapi pametulia na kwenye fursa za Biashara?

Asante🙏
 
Unatutangazia nini sasa? Kiwanja, nyumba!
 
Mmmm sasa umeajiriwa utawezaje kujipangia iwe hapa kwa muda mrefu ?? Sijaelewa hapo
 
Hii nchi, uelekeo ni mmoja tu;
  • Biashara
  • Mkulima
  • Muajiriwa

Kwa mujibu wa uchumi wetu, huwezi kufanya yote au mawili kwa wakati mmoja KAMA SIO MWIZI, FISADI, BADHIRIFU au MDHULUMU HAKI za watu.

Wengi ukiwaondoa kwenye ajira, biashara zao zinakufa pia....kilimo chaliii!

Ukisema wapo wanaotamalaki, kamuulize Manji kilichomkimbiza nchini, Silent Ocean kuwa mufilisi n.k

Tafuta sehemu ya kuishi na familia, kisha uchague AJIRA au FURSA
 
Kwa kuishi na utulivu nenda Iringa.
 
Nakushauri angali karibu na kwenu...Dar ni ya kichoko kama umeajiriwa Dar sio sehemu salama kwanza mda wa kwenda na kurudi ila kama biashara Dar magoli mwanzo mwisho.

Angalia karibu na kwenu Tanga ,Iringa ni best kama unategemea ajira tu kwa sababu maisha yapo chini sana.

Karibu na kwenu ili ukifa usisumbue watu gharama ya kusafirisha maiti.
 
Heshimu sana kazi hiyo uliyonayo Sasa

Biashara ni ngumu sana inaleta stress na kukausha Damu mwilini

Kama bado mwajiri anakupenda usijiroge kuacha kazi eti kisa unataka kuanzisha Biashara

Biashara zina wenyewe na zinahitaji muda mpaka uanze kuona faida
 
Hapana sina mpango wa kuacha kazi. Mara nyingi ninapo hama ki Kazi huwa nahama na familia kwaiyo. Naitaji kwa Sasa familia yangu itulie sehem moja hata kama nikihama mie ki KAZI mkuu nazani umenielewa
 
Umewaza mbali sana mkuu kwamba nikifa nisisumbue watu😹
 
Hapana sina mpango wa kuacha kazi. Mara nyingi ninapo hama ki Kazi huwa nahama na familia kwaiyo. Naitaji kwa Sasa familia yangu itulie sehem moja hata kama nikihama mie ki KAZI mkuu nazani umenielewa
Hapo nimekuelewa

Kama ni hivyo mbona hilo halihitaji hata ushauri, kama watoto hawajaanza shule Endelea kuhama nao, kama wameanza waache Dar Es Salaam ambako ndiko kwenye bandari na uwanja wa ndege mkubwa kuliko viwanja vingine vyote TZ
 
Dar ndiyo mpango mzima. Mikoani kulishana vumbi tu
Mmmm sasa umeajiriwa utawezaje kujipangia iwe hapa kwa muda mrefu ?? Sijaelewa hapm

Hapo nimekuelewa

Kama ni hivyo mbona hilo halihitaji hata ushauri, kama watoto hawajaanza shule Endelea kuhama nao, kama wameanza waache Dar Es Salaam ambako ndiko kwenye bandari na uwanja wa ndege mkubwa kuliko viwanja vingine vyote TZ
Shukulan
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…