Nimechoka kuhangaika ila akilini mwangu Nina mawazo makubwa!!!!

winner100

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2016
Posts
325
Reaction score
209
Nafikiria kuanzisha clinic au hospitali. Ila sina pesa , nafikiria kuanzisha vijicenters vidogo vya kupika na kuuza mihogo hii ya kukaanga na chachandu ili kuongeza kipato cha kila siku baadae kufanya biashara kubwa !!!!

Zitakazo nipa faida na kuanzisha hospitali
Sasa wanajamiii je kwa hiyo biasha ndogo nitaweza kupata faida itakayoongeza mtaji wakufanya biashara zingine!!!

Naona wanaopika maisha yao ni Yale yale sijui Mimi nitatoka kweli hii biashara ??????

Naombeni mnitie moyo na kunipa mawazo mengine ya kufanya nikuze mtaji na kufikia malengo yangu!!!!
 
Yaapp utafanikiwa ndugu. Ila fanya utafuti vizuri wa hizo center kama zitauza biashara yako ya mihogo kwa kasi bila kulaza mihogo na kusababisha hasara. Nakushauri, lenga kwenye shule za msingi na sekondari, pia uza juice za matunda au aice cream kama uko mikoa ya joto kama kisukumio kwa bei afodabo. Nakumbuka pale mnazi mmoja primary kuna jamaa alikua anauza muhogo na juice tamu sana kwa bei afodabo sana, mpaka akafahamika kwa jina la "said mihogo"
 
Kuna jamaa alipost kuhusu muuza bajia...akiuza bajia 250 kwa siku kwenye shule kwa mfano kwa bei ya sh 200 anapata elfu 50 kwa siku 20 za kazi kwa mwezi ana 1m. Vivyo hivyo ukiwa sehemu nzuri.ukaweza kuuza vipande 200 kwa siku utafika mbali. Chamsingi usikate tamaa kabla hata ujaanza fanya ikifeli kuna abc utajifunza zitakusaidia katika kufikia ndoto.

"Never give up on your dream just because of the time it takes to accomplish it, the time will pass anyway" by Unkown
 
Aiseee Mungu awabariki kwa ushauri wenu!!!
 
Cool advice!!! Thanks a lot.
 
Mkuu wehoodie elfu 50 ni faida au mauzo ya Siku!!
 
Mauzo mkuu lakini ni mfano tu kiuhalisia kutegemea na eneo inaweza kuwa zaidi ya hiyo. Kwa mfano unaweza kuuza labda 500 au buku kama wale wa coco. Fikiria wale jamaa akiuza pisi 100 tu ana 100,000. Kimsingi jitahidi ufanyie sehemu yenye watu wengi na zingatia usafi.
 
Unataka kuingia kwenye biashara for wrong reason hebu jitafakari kwanza maana biashara inahitaji guts za uthubutu wewe akili yako bado haijawa tayari kwa biashara maana uoga wakoo ni kukaa kuajiriwa tuuu
 
Cha msingi katika maisha usiangalie wale waliombele yako kimaisha wakakukatisha tamaa, ndugu kimbio mbio zako na umalize ukiwa mshindi, usikate tamaa anzia hapo hapo ukiwa na plan baada ya muda fulani utakuwa sehemu nyingine.
 
Freelancer!! Me sipendi kuajiriwa!!!
Hii kauli ya kusema kwamba naona maisha ya wanaouza mihogo hayana unafuu tayari inaonyesha bado huna attitude ya kijasiriamali. Nilitegemea utasema nimechunguaza nimegundua kwamba wanakosea hiki ndo maana hawafanikiwi kwa hiyo mimi nitafanya hivi kuhakikisha nafanikiwa hiyo ndo spirit anayotakiwa kuwa nayo mjasiriamali
 
Kikubwa ukiamua kuwa mjasiriamali ni lazima uwe risk taker,na pia ukitaka kuanzisha biashara kikubwa ambacho unatakiwa ukifanyie upekuzi ni kwenye masoko wanataka nini,kuna shortage ya product ipi ambayo clients wanaitafuta,then fanya mchakato wa kuanza kusupply hiyo bidhaa.....kwa mihogo tafuta right place ambapo wateja wa bidhaa hiyo utawapata vizuri.
 

Safi kabisa.
 

namuunga wehoodie ,.,.,., pia naongezea `biashara ya mihogo hata ktk vituo vya daladala kuna wateja.,.,eg Mkwajuni``
 
Kwenye watu hapakosi kitu, mbarikiwe asee na wengine tunafaidi ushauri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…