Nimechoka kuishi kwa wazazi, naombeni ushauri

Nimechoka kuishi kwa wazazi, naombeni ushauri

Toni Toni

Member
Joined
Nov 19, 2022
Posts
5
Reaction score
22
Shikamooni wakubwa zangu mdogo wenu naomba ushauri kidogo kutoka kwenu...

Mimi ni kijana mwenye miaka 24 naishi hapa dsm ila mpaka muda huu bado naishi nyumbani kwa wazazi, kwa umri wangu nshaona kuwa najiendekeza sana mana mpaka sasa ningekuwa najitegemea na mimi niwapunguzie mzigo wazee.

Ila kinachonkwamisha ni kwamba sijui ata nkiingia mtaani ntafanya inshu gani mana sina ata uzoefu wa harakati za kitaa.na ata mtaji wa kuanzia biashara yoyote sina

Kidogo nna ujuzi wa kompyuta tu. Bado npo chuo ndo nimeanza ngazi ya cheti mwaka huu..

Tuanzie hapo wakubwa zangu kwa mwenye ushauri wowote?.
 
Sasa kama huna kitu unaondoka uende wapi? Kikubwa jichanganye na wazeiya ukiotea mishe jioni unawatoa nyumbani kwa ajili ya riziki ya kesho kwa style hii hutoonekana mzigo
 
Tulia hapo hapo kwenu
Anza tafuta hela ukiwa kwenu umtunze mama yako..
Usikimbilie kuhama ukipata hela ukahonge Malaya ..huku .ana yako bado ana matatizo...

Umesomea computer Anza kufanya kazi za graphics..jitangaze online unapata hela unamtunza mama yako
 
Back
Top Bottom