Nimechoka kusoma bora nitafute hela tu

Nimechoka kusoma bora nitafute hela tu

Mr Equalizer

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2013
Posts
611
Reaction score
727
Nilipomaliza kidato cha nne nikajaribu maisha yakawa magumu nikaona bora nirudi shule labda hali ingebadilika hivyo nikajiunga na high school baada ya kumaliza nikarudi kitaa kutafuta maisha yakawa magumu tena.

Nikaamua kwenda chuo kikuu nikasoma nikamaliza shahada ya kwanza lakini bado maisha ni magumu sana.

Juzi niliamua kurudi chuo kikuu, lakini sina uhakika kama elimu itanisaidia kumaliza huu ugumu wa maisha, labda nikomae tu kitaa nifute pesa. Elimu ya bongo inatesa sana lakini haitukomboi kwenye umaskini.
 
Komaa kitaa ata ukirud shule ukimalza tena bado maisha yapo vilevile komaa lazma utatoboa
 
Ulivyoandika ni kama vile HUJAPATA KAZI lakini nakukumbusha tu MKUU WEWE NI MWALIMU. Rejea uzi wako wa 2014 hapa chini na nimeweka red kwenye maeneo muhimu

Wana jamvi kwanza nawapongeza kwa kumaliza vizuri mwezi wa ramadhani.Lakini kwa baadhi yatu sisi Walimu sikukuu hii imekuwa si ya furaha kwani mpaka sasa hivi hatujapata mishahara yetu, wakati wenzetu wamepata tangu tarehe 25. Kwa kweli tumesikitika sana ukizingatia tunaishi mazingira magumu sana huku vijijini ambako serikali imejenga shule za Kata. Huku hatuna maji, umeme, hata net work ya kutuwezesha kuwasiliana na ndugu zetu haipo .Tukiwauliza watendaji wa halmashari nao wanasema hawajui kilichotokea hatuna mtu wa kutusaidia. Serikali kuu iko mbali sana na sisi.Tunapenda sana kuitumikia serikali lakini hii imetukatisha tamaa kabisa.
 
Pamoja ya kuwa tafsiri ya University ni chuo kikuu ila kwangu mtu akitaja chuo kikuu nawaza UDSM tu sijui ni kwanini
 
Ulivyoandika ni kama vile HUJAPATA KAZI lakini nakukumbusha tu MKUU WEWE NI MWALIMU. Rejea uzi wako wa 2014 hapa chini na nimeweka red kwenye maeneo muhimu

Labda best frnd wake alitumia Jf account yake kupost.
NB::: hata Mimi nimetumia account ya ndugu yangu kuku reply wewe #kipilipili .
 
Nilipomaliza kidato cha nne nikajaribu maisha yakawa magumu nikaona bora nirudi shule labda hali ingebadilika hivyo nikajiunga na high school baada ya kumaliza nikarudi kitaa kutafuta maisha yakawa magumu tena
Nikaamua kwenda chuo kikuu nikasoma nikamaliza shahada ya kwanza lakini bado maisha ni magumu sana.
Juzi niliamua kurudi chuo kikuu ,lakini sina uhakika kama elimu itanisaidia kumaliza huu ugumu wa maisha ,labda nikomae tu kitaa nifute pesa.Elimu ya bongo inatesa sana lakini haitukomboi kwenywe umaskini.

Ndugu yangu usiwe na wasiwasi soon tu utavushwa,au kama sivyo ipo safari ya matumaini,tumaini jipya n.k kuwa na subira punde tu
 
Matajiri wengi hawana shule kichwani na ila wana akili. Nyie mliosoma mmefundishwa uchoyo na ulimbukeni kuwa kazi nzuri ni kuajiriwa ili uibe! Hatuna mawazo ya kuanzisha vya kwetu
 
pamoja ya kuwa tafsiri ya University ni chuo kikuu ila kwangu mtu akitaja chuo kikuu nawaza UDSM tu sijui ni kwanini
hata mimi nna mawazo kama yako... Mi nimesoma udsm Enzi ile nikienda kitaa nikiulizwa unasoma wap nlikua nasema chuo kikuu
 
Hawa ndio baadhi ya walimu wanaoondoka ktk ajira pasipo ruhusa ya mwajiri kwa gia ya kwenda kuongeza elimu bahati mbaya sasa hv kuna mfumo wa ajira serikalini mwalimu akitoroka hawezi ajiriwa pengine na kwa kuwa hakujiandaa na life la mtaani inakuwa Sheeedah.

Na anaona akaongeze "Master" sijui ili AMASTE nn, mwisho wa siku anajutia maamuzi ns kusema maisha ya kusoma yamemshinda na anatapatapa....
 
Ulivyoandika ni kama vile HUJAPATA KAZI lakini nakukumbusha tu MKUU WEWE NI MWALIMU. Rejea uzi wako wa 2014 hapa chini na nimeweka red kwenye maeneo muhimu

Basi huyu jamaa ni mtu wa kulialia tu miaka nenda rudi.
 
Back
Top Bottom