Nimechoka maisha ya ughaibuni

Phobia

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2021
Posts
1,156
Reaction score
1,819
Ama hakika maisha ya ughaibuni kwa ujumla yamenichosha jamani yaanj sio poa kabisa yaani kutwa kushinda uko pekee yako hamna vijiwe vya kahawa na kashata kama huko bongo yaanj kutwa kufanya kazi saving ni kipengele sana kwasababu unafanya kazi mara ulipie mortgage, mara ilipie car rent hamna kuwapiga watu mizinga kama huko kwenu

Baada maisha ya new Harlem New York kunishinda nimeamua kuhamia Wisconsin angalau nipunguze Gharama ya maisha kidogo maana maisha yalikuwa sio poa viwanja vya starehe ni gharama sana nataka nipambane kidogo nihamie Kentucky nika hang na waAfrika wenzangu angalau nitaenda kupata miguu ya kuku kama huko uswahilini aisee
 
Winter hii mkuu. Kamata demu wa kitasha utulie.
 
Nenda Mwalimu, unatuondolea stimu

- Juma Nature
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…