Nimechoka na mashugamami...

stevoh

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2011
Posts
2,921
Reaction score
1,105
Tatizo langu nahisi linazidi kila nikimpenda mwanamke namkuta amenizidi UMRI mpaka nachoka nimeingia kwenye mahusiano wa kwanza tulikua miaka sawa ila tukashindwana wa pili kanizidi miaka miwili alafu tukazinguana sasa niko SINGO ila naogopa kuingia kwenye mahusiano tena kisa UMRI.

CANCELING PLEASE
 
Muwe mnaandika kiswahili si lazima kuandika kiingereza ilhali hujui..ujuaji mwingi mbele kiza..
Thread yako yaonesha ww bado ni kijana mdogo sana..komaa na maisha kwanza wapenzi watakuja tu..na ukumbuke UJANA NI MOTO...
 
kama kwa tofut ya miaka miwili unamwita sugamami, je angekuwa na umri wa mama yako ungemwitaje? Unaonekana umekurupukia neno usilolijua! Kubadilisha wanawake si ujanja maana si nguo ubadilishe kila ichafukapo! Usitudhalilishie dada zetu! Jipange kwanza!!!
 
'cancelling' please....# nimeipenda hii.
mbona hujasema umetembea na mashugamami wangap kias cha kuchoka hivyo..
 
counselling mdau
 
Acha tamaa inaoneka una haha na wanawake badala ya kujikita kwenye kutafuta pesa,acha hizo dogo.
 
Unaelewa maana ya sugarmumy au umesema tu na wewe uonekane umo??
 
Muwe mnaandika kiswahili si lazima kuandika kiingereza ilhali hujui..ujuaji mwingi mbele kiza..
Thread yako yaonesha ww bado ni kijana mdogo sana..komaa na maisha kwanza wapenzi watakuja tu..na ukumbuke UJANA NI MOTO...

Nimekupata kaka ila nadhan ujumbe umeupata!
 
Sawa lakini wewe sijui umeoa?
 
'cancelling' please....# nimeipenda hii.
mbona hujasema umetembea na mashugamami wangap kias cha kuchoka hivyo..

Mpaka sasa ni relationship 3 tu na zote hazijadumu mda mrefu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…