Nimechoka, naenda kununua gari

co fm

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2016
Posts
1,541
Reaction score
2,487
Japokuwa wanasema usifanye kitu kwa kuiga au kuhisi watu watakuonaje ila inafika point unaamua ufanye tu ili upate amani. Mimi ni kijana naishi Dar mshahara wangu ni kipato cha kati tu.

Sasa hapa ninapoishi vijana wenzangu wote wana magari kasoro mimi sasa naona kama najifeel inferior sana, niliwahi omba ushauri humu JF wengi walinishauri nisinunue gari kwa kufuata mkumbo ila sasa naona uzalendo umenifika hapa.

Nimepanga kununua gari nina akiba yangu ya 4M bank na ninaenda kukopa 3.5M naenda kununua ist. Kwa mliokwisha kuwa na magari ya mikopo staili hii ni changamoto gani ninaweza kukumbana nazo na je utakuwa uamuzi sahihi?
 
Trust me. Kwa DSM usipokuwa na gari status yako ni ndogo sana. Fedheha ya kuwa na deni ni ndogo sana ukilinganisha na kuwa na gari. Nilienda kwene kikao cha harusi wote walikuja na magari kasoro mimi na ninavuja jasho balaa. Nilikaa kwa unyonge sana siku hiyo.

Nilivotoka nikasema sasa sisikilizi mtu nilivoamka nikawahi bank nikakutana na dada wa mikopo nikamwambia nataka kukopa mil. 20 nikapewa mkopo within 2 weeks. Nikadaka ndinga. Guess what? Hio milioni ishirini niliipata baada ya miezi mi4. Niliitwa somewhere kuna dili la maana nikatinga na ndinga yangu suti ya maana nikasaini mkataba fasta. Maisha yakaendelea.

Acha kusikiliza watu humu hatujuani. Hata mimi niliyoyaandika usiyape kipaumbele sana utaumia.

Asalamaleko
 
Maisha ni hayahaya, we fanya kile unachòona kitakupa furaha tele moyoni .
 
Nunua gari, fanya kitu rorho inapenda acha kuumiza moyo wako.... DUNIANI KWENYEWE TUNAPITA SASA CHUKUA USAFIRI UPITE KWA KASI.

Narudia tena Dont fight yourself..............
 
Sababu zako za kununua gari ni dhaifu sana, uwe na malengo ya zaidi na hilo, gari Dar inahudumiwa kwa average ya 20,000 kwa kila siku mwezi ni 600k, mshahara wako kama ni 900k monthly, siunaona unaingia kwenye dimbwi la 'urban silent poverty'
 
Mzee baba, wewe fanya hivi, kwa sababu unahitaji gari na kama mshahara wako ni mdogo, ukifanya kwa mkumbo ni kwlei baadae mambo yatakuwa magumu sana, wese na matengenezo. Chukua uamuzi, hiyo m4, kama unakopa kopa kiasi kidogo mno labda hata m1 au 2, bado utapata ist used kwa m6, jitahidi ufanye uraise hela basi uingie hata bolt au uber ili week end unaraise hela kidogo ya mafuta labda na jioni ukitoka job unapigia mishe kidogo.
 

Asante mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…