Nimechoshwa na U.T.I naombeni msaada

mwanaume ni kazi sana kupata UTI. nakushauri utafute dawa za kichocho unywe.
 
Mkapme wote na dawa mkipewa kunyweni halaf km mnavimeo nje mpumzike ! Na mnywe maji sn ht hadi ltr 5
 
Jamani ebu nipeni ushauri kweli naweza kupona U.T.I na je ni njia gani nifuate nimechoka mwenzenu kupoteza hela zangu kila siku hosptali!
Nenda hospital inayoeleweka waelezee dawa gani umetumia na mara ngapi imejirudia. Ikilazimu inabidi upigwe sindano flani inayochomwa ktk mishipa ya damu moja kwa moja. Kuna uwezekano mkubwa mara zote inakuwa haujapona kabisa . Unamaliza dozi vizuri bila kukatisha ukipata nafuu? Au haurki ruki masaa ya kunywa dawa?
 
Jamani ebu nipeni ushauri kweli naweza kupona U.T.I na je ni njia gani nifuate nimechoka mwenzenu kupoteza hela zangu kila siku hosptali!
Unapoanza kunywa doz mpe na mpenz wako na michepuko yako yote....ili mpone wote ndo muanze tena ngono zembe
 
Wakina dada lazima mjue dawa za huu ugonjwa
 
U T I inatokana na kushindwa mgt ya usafi(kinyesi) unatawaza mbele na nyuma Kwa mkono huo mmoja mchafu. Hatavyo, unaweza kupata Kwa kufanya mapenzi na mwenye UTI. Pata ushauri Wa Daktari ili ujikinge otherwise utamaliza madebe ya dawa matokeo yake utaumwa figo na baadae umauti huwezi kupona.
 
Pia kwa ushauri mwingine kama unaishi na girlfriend au mke jaribuni kwenda wote hospitali mkacheki inawezekana unachukua maambukizi kutoka kwa mwenza wako.
 
pole sana kaka. Jitahidi ukiamka asubuhi kabla ya kula chochote katakata matango ule baada ya hapo kunywa maji mengi sana. fanya hivyo asubuhi na jioni then ulete mrejesho baada ya wiki. pia angalia sana vyoo unavyotumia huenda sio visafi. jitahidi kusafisha kabla ya kutumua na kama ni vya ku share hapo ni tatizo.
 
Usafi muhimu
naoga mara4 kwa siku
nabadili chupi mara4
sinawii sabuni kwenye k
nikienda chooni namwaga maji nikimaliza haja nanawa namwaga maji then najikausha ..
nakunywa maji lita 3 au na nusu kwa siku.
sijipulizii pafyumu ukeni wala sipaki lotion, wala misk wala madura stick...

napiga deki chooni kutwa mara3
hatukai wengi.
tatizo nini?
 
Mkuu kama bado hujapona nakushauri nenda hospital moja inaitwa megra specialists clinic, ipo pale kivulini upande wa kushoto karibu na mataa ya superstar, ukipita mlimani city. Hapo utapona, niamini mimi
 
Kama bado inakuzingua nenda hospitali wanaotoa vipimo vya culture ndio suluhisho la tatzo lako.
 
Kwa maisha ya TZ kubadilisha na routine ya usafi unatufix. But take care na wapenzi wako.
 
Uwe unakunywa maji mengi

Nilipopata UTI nilifanya udadisi nikagundua nakunywa soda kwa kiwango cha juu sana kuliko navyokunywa maji.
Nikapunguza soda nikawa nakunywa maji mengi.

Sikutumia dawa nyingine yoyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…