Wewe dada angu, una bahati kwani umeleta JF ndo penyewe. Kuna wengine hawajui pa kukimbilia wala wa kumueleza kwa hiyo tuliza moyo. "Acha mawazo ya kujisikia maisha bila mwanaume hayawezekaniki". Sasa ndo muda wako wewe kuonyesha kuwa umekomaa kifikra. Pigana kwa njia sahihi, ondoa hayo mawazo ya kujilaumu kwa mambo yaliyopita, songa mbele.
Jitahidi tu kuweka mipango yako vizuri, nenda kanisani kila jumapili au msikitini kila ijumaa au jumamosi sali na rudi nyumbani jipange kwa kazi zako.
Wanaume wapo wengi tena sana, atakuja atakayematch nawewe. Onyo, usifanye haraka kumpata kisa umemiss mambo fulani, vumilia jiweke sawa kila idara. Nakuhakikishia ndani ya mwaka mmoja utakuwa unawaza vitu vingine kabisa kama kufungua mradi wa ..... maeneo fulani.
Nakutakia kila kheri, najua hutapuuzia kuchukua mchele na kuacha pumba.