Nimedhurumiwa

obi's

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2011
Posts
233
Reaction score
40
Jamani habari za majukum? Poleni. Jamani naombeni msaada, kuna jamaa mmoja ni mcongo man amenidhurumu tsh.500000. Amerudi kwao hapokei simu yangu. Msaada jamani nifanyeje?
 
mkataba wowote kuwa ulimpa hizo pesa
collateral yoyote
unajua anakokaa au anatokea wapi
mlipeana katika mazingira gani ya kiurafiki au kikazi
na kama kikazi under which contract
 
Ela Ndogo Sana hiyo utapoteza ela nyingi na muda mwingi kama utaamua kuifuatilia.
 
Jamani habari za majukum? Poleni. Jamani naombeni msaada, kuna jamaa mmoja ni mcongo man amenidhurumu tsh.500000. Amerudi kwao hapokei simu yangu. Msaada jamani nifanyeje?

Kama mlikopeshana kiholela, sahau hiyo hela.
 
Unatoaje hela yote hiyo kwa watu ambao huna uhakika nao,
kwanini kufanya biashara na wakimbizi mkuu.
ungekuwa umeituma kijijini kwenu ungeweka heshima hadi mwisho wa maisha yao.
hiyo hesabu tu kama sadaka.
 
Jamani habari za majukum? Poleni. Jamani naombeni msaada, kuna jamaa mmoja ni mcongo man amenidhurumu tsh.500000. Amerudi kwao hapokei simu yangu. Msaada jamani nifanyeje?

Pole sana!!
 
cha kukushauri nenda ukaripoti kituoni kwani lazima gtarudi.na kama sheria inavyosema mtu akiwa anadaiwa ikipita miaka sita na hamna shauri lolote mahakamani au polisi hilo deni limeshafutwa hautaweza kumdai tena.
 
Jamani habari za majukum? Poleni. Jamani naombeni msaada, kuna jamaa mmoja ni mcongo man amenidhurumu tsh.500000. Amerudi kwao hapokei simu yangu. Msaada jamani nifanyeje?

Kumfuatilia mtu aliyerudi Kongo mpaka umpate, umpeleke mahakamani utakuwa umeuza ng'ombe kwa kesi ya kuku. Vumilia tu rafili labda atarudi baadaye.
 
Jamani asanteni kwa ushauri mzuri. Mazingira ya pesa hiyo, huyo mtu alikuw mwanza akishughulika na mambo ya minala, akiwa ndie kiongoz na mmiliki wa kikampuni cha intertec co. Walikuwa wakifanya kazi china ya gtl. Kwa kuw nilikuwa nafahamiana nae, gari yangu ilitumika ktk kaz zake, mwanzon alikuwa ananilipa bila shida, ila ikafikia mahari akasema pesa ameishiwa hivyo niendelee kumfadhir gari mpaka kazi amalize ndio atanilipa. Nilikubar deni lilifika m1 akalipa nusu, nusu ndio ameingia mitini. Asante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…