Nimefanikiwa kupata ardhi ya ukubwa wa ekali 8,nizitumieje?

Nimefanikiwa kupata ardhi ya ukubwa wa ekali 8,nizitumieje?

shangwe shangwe

Senior Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
108
Reaction score
24
wadau nimefanikiwa kupata na kumiliki ardhi ya ekali 8. Sasa naomba msaada wenu wa kimawazo namna kuitumia ipasavyo ili niweze kuuepuka umaskini.
 
wadau nimefanikiwa kupata na kumiliki ardhi ya ekali 8. Sasa naomba msaada wenu wa kimawazo namna kuitumia ipasavyo ili niweze kuuepuka umaskini.

jipange uandike andiko lako vizuri. Fikiria wewe ndiye uliyeulizwa swali la jumla hvyo unajibu nini?
Kila ardhi ya eneo lolote lile inatofautiana kimatumizi.
Ila nikuulize kwa nini ulitafuta hiyo ardhi?
 
wadau nimefanikiwa kupata na kumiliki ardhi ya ekali 8. Sasa naomba msaada wenu wa kimawazo namna kuitumia ipasavyo ili niweze kuuepuka umaskini.

Dadavua zaidi ili usaidiwie vizuri, kwa mfano hiyo ardhi imeipata wapi? (yaani ipo sehemu gani? Dar au wapi?), ipo mashambani au mjini? nini vipo karibu yake (eg Maji (mto/mfereji, mlima, bonde, n.k au barabara, shule, kanisa, etc) na mambo mengine. Ukiweza kudadavua naweza kukusaidia project planning...
 
Iko siku humu jamvini tutaulizwa eti leo nile nini?au eti leo nivae nini?
Mdau..wewe ulipokwenda kununua hiyo ardhi ulikuwa una mpango gani nayo?eka nane za wapi,jangwani,bondeni,mwanza,arusha,moshi au wapi?swali lako liko too general sana!
 
Dadavua zaidi ili usaidiwie vizuri, kwa mfano hiyo ardhi imeipata wapi? (yaani ipo sehemu gani? Dar au wapi?), ipo mashambani au mjini? nini vipo karibu yake (eg Maji (mto/mfereji, mlima, bonde, n.k au barabara, shule, kanisa, etc) na mambo mengine. Ukiweza kudadavua naweza kukusaidia project planning...

thanx,ardhi hiyo nimepewa,iko maeneo jirani na makazi ya watu,mto na ni jirani na maeneo yaliyopangwa kuwa makao makuu ya wilaya mpya ya Buhigwe mkoani kigoma.
 
Kama ipo kigoma wapoti basi muone brother k au bizmana wakupe mbegu za mawese upande michikichi.
 
jipange uandike andiko lako vizuri. Fikiria wewe ndiye uliyeulizwa swali la jumla hvyo unajibu nini?
Kila ardhi ya eneo lolote lile inatofautiana kimatumizi.
Ila nikuulize kwa nini ulitafuta hiyo ardhi?

Mkuu hata mi sijamuelewa ni sawa mtu kapika chakula alafu anawapigia watu simu anawaulize 'hiki chakula nilchopka nikifanyeje?'
 
Jibu maswali ya wadau upate ushauri.
Ninaomba hapa jamvini tujifunze kuchukuliana na kuvumiliana. Hata kama ningekuwa mimi ningeona nimepotea njia. Mtu kauliza swali la ufanhamu halafu anashambuliwa kama nzinge! Mwiho wake tutampoteza huyu mwenzetua. Anaweza kuona jamii hii siyo yake. Hakuna mtu anyeenda kwenye kujumuika ili apate dhihaka na kudharauliwa.Hajialishi ardhi kapata kwa, kununua ama zadi. Kilicho dhahiri ni kwamba hana idea afanye niozni. Badala ya kumshambulia ni kumpa maswali ya mwongozo. Na kama hujui unanyamaza.Kumbuka hakuna mjuzi wa mambo yote wakati wote, mahala pote. This is jamii forum. We should learn how to complement each other, espcially when a person has declared to have low knowledge on something. Nimeumia sana kwa sababu huyu mtu hajaja na arrogance. Amekuwa submissive kwambaa anahitaji ushauri. Kwa nin mnamdaka namna hiyo?Naomba tujaribu kuona si vyema kufrustrate peaceful people kama huyu kijana.Naomba mwenye kujua aseme naye kwa upendo.Usiyejua nyamaza.Hutaki ku share naye hata dharau na dhihaka zako usimshirikishe.NATAMANI TUJENGE JAMII FORUM YENYE MLENGO WA KUSHIRIKISHANA NA KUSAIDIANA.
 
Back
Top Bottom