Nimefanikiwa kutengeneza majani ya chai ya asili, so sweet, nutritious and energetic

adriz

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Posts
12,207
Reaction score
26,521
Moja kwa moja kuokoa muda..

Mimi sio mpenzi wa kutumia majani ya chai ya dukani mara nyingi napenda kutumia chai ya mchaichai,baada ya kupitia nyuzi mbalimbali humu zinazohusu mti wa mlonge na faida zake nikahamasika sana kutengeneza majani ya chai ya mlonge.

Nikaingia YouTube na gugo na kusoma makala mbalimbali zinazohusu mti wa mlonge na namna bora ya kuyaandaa majani yake kwa matumizi mbalimbali hivyo nikafuata maelekezo na kufanikiwa kutengeza majani yake ambayo natumia kama chai kwa kuchanganya na maji ya moto kutumia kama chai na mara nyingine kuchanganya na uji.

Matokeo baada ya kutumia.
1.Mwili mzima unapata nguvu na msimko wa ajabu(vibe) mara tu unapomaliza kutumia wakati mwingine jasho linachuruzika.

2.Mimi mfanyaji wa mazoezi ya push ups siku mara siku ninayotumia hicho kinywaji hali inakua tofauti napiga mara mbili ya idadi nitapigwa kikawaidia nikaimagine nguvu hizo ningezihamishia sehemu nyingine kwenye sekta ya mzabzab naiona Tz ya viwanda ya Anko Magu

3.Akili inakua verry active

4.Baadhi ya homa ndogo na uchovu wa mwili hukatika husisha kwa haraka

5.Matokeo mengine ambayo wenyezi Mungu pekee anajua .

Kwa sasa nimefanya ndio chai yangu rasmi na nimejiongeza na kuiupdate kwa kuchanganya na tangawizi(kavu) na iriki na kuisagia pamoja .



Nb:Lengo la uzi huu sio biashara kwani sijafika kiwango cha kutengeza mwingi na kuwa na vitendea Kazi imara ila malengo ya uzi huu ni kutoa maarifa na kuongeza maarifa kupitia wachangiaji mbalimbali.

#UziTayari
 
Baadhi ya comment za wana Jf zilizonipa hamasa ya kutengeza ma

 
Ni nzuri sana ila usipende kunywa kila siku hiyo,huwa inashusha sana presha hiyo
 
Mlonge ni mzuri sana kwa afya, ila sasa hiyo sio chai labda kama unachanganya na majani ya chai
 
Ni nzuri sana ila usipende kunywa kila siku hiyo,huwa inashusha sana presha hiyo
Yah ,sinyi kila siku huwa kila baada ya siku mbili au tatu siku nyingine nasubiri wiki wakati nikiiandaa nyingine.
 
Mlonge ni mzuri sana kwa afya, ila sasa hiyo sio chai labda kama unachanganya na majani ya chai
Sichanganyi na majani ya chai sitaki kuongeza kemikali mwilini ,huwa natoa kwenye uji nakorogea au maji ya moto naweka na chujio napata chai safi na tokea jipya niwekea iriki na tangawizi haina haja na majani ya chai.
 
Tanzania ya viwanda😂😂😂
Hii inchi ina mapori mengi hayana kazi hivyo sera ya Magu ikizelezwa inavyotakiwa mapori yatabaki historia watu wengi tutapata nguvu kazi za kulima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…