Nimefilisika jamani

Mtaji wangu umekata mpaka kupelekea kuuza kuku wa mayai wapo 540(mia tano arobaini),bado wiki mbili waanze kutaga..nawauza kwa bei ya jumla sh.MILLION 3.
SABABU.
Hii ni baada ya kukosa hela ya kuendelea kuwahudumia baada ya kusimamishwa kazi..

Ungetaja na mahali unakopatikana, ikibidi na mawasiliano yako ya simu! ili kuwarahisishia wale wateja ambao ni vigumu kukupata kupitia PM.

Pole sana.
 
Mtaji wangu umekata mpaka kupelekea kuuza kuku wa mayai wapo 540(mia tano arobaini),bado wiki mbili waanze kutaga..nawauza kwa bei ya jumla sh.MILLION 3.
SABABU.
Hii ni baada ya kukosa hela ya kuendelea kuwahudumia baada ya kusimamishwa kazi..
Wakati kama huu hutakiwi kupaniki!

Unakaa chini, unalia kidogo, unapangusa machozi, halafu unasimama unatafuta sehemu tulivu unawaza yafuatayo:-

1. Nimeachishwa kazi ndio, je mi ndo wa kwanza kukumbwa na hili? Jibu ni Hapana

2. Hivi wanaokutwa na changamoto kama hizi wanakuwa wamejipanga? Jibu ni Hapana kwa walio wengi!

3. Wakati naendelea na mengine, Nina nini mkononi? Jibu, una kuku 540! Haaah! Wengi hivi! Aaah...kumbe nina utajiri mkubwa hivi!

4. Lakini, kazi ndo ilikuwa inawahudumia hawa kuku!!... Ndio, hilo ni kosa maana ilitakiwa ifike mahali hawa kuku waanze kujihudumia wenyewe (mradi ujiendeshe)

5. Hapa unagundua ni kweli ulifanya kosa kidogo kuendelea kutumia mshahara kuendeshea project iliyokwisha simama...wala sio kosa kubwa hili!

6. Baadaye unajiuliza, hivi anayesimamishwa kazi na Hana hata kuku mmoja inakuwaje? Lazima atafanya atakachoona rahisi kwake lakini ki ukweli atayumba sana na atahangaika maana huyu hana chochote mkononi!

7. Sasa nataka niuze kuku wote! Ili iweje? Nifanyie nini hela hizo? Yaani kushindwa kuwahudumia ndo niwauze wote! Hapana!

8. Ukisha sema hapana, unapiga mahesabu ya chakula cha kuku na matunzo mengine na pesa kidogo ya familia kwa kipindi unachohisi kinafaa! Labda mwezi mmoja

9. Unaingia sokoni unajua soko la kuku likoje, unapiga mahesabu, unapata idadi ya kuku watakao kupatia hicho kiasi cha pesa unacho hitaji!

10. Ukishawauza hao wachache, utakuwa umepoteza kazi moja na kubaki na kazi nyingine ya kukuza mradi wako!

Shukuru Mungu wewe unapa kuanza kabisa! Wengine wanaachishwa kazi hawana hili wala lile!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uncle Jei Jei,
Brilliantly. Huyu ndiye moja ya great thinkers. Asanteni na wengine mluichangia positively. Hao wachache wanaokebehi wajue maisha ni kupeana vijiti. Na kubwa zaidi ukiwa umesimama katika mtari ukiwa namba moja siku ukiambiwa nyuma geuka yule no mwisho ndiyo anakuwa wa kwanza.
 
Mtaji wangu umekata mpaka kupelekea kuuza kuku wa mayai wapo 540(mia tano arobaini),bado wiki mbili waanze kutaga..nawauza kwa bei ya jumla sh.MILLION 3.
SABABU.
Hii ni baada ya kukosa hela ya kuendelea kuwahudumia baada ya kusimamishwa kazi..
Pole sana fuata ushauri wa uncle jay jay kingine usijisikitie sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…