Nimefiwa na Mama Mzazi

Pole sana mungu akupe nguvu na faraja kwakipindi hiki kigumu kwako!
 
Wakuu, naomba kuchuwa nafasi hii kuwashukuru nyote kwa ushirikiano wenu na kuonyesha kujali kwenu. Kuna ambao wameniandikia email na wengine PM, lakini kwa bahati ghafi sikuweza kuwajibu, ni matumaini yangu kuwa wataelewa situation niliyokuwa nayo...!

Nilikuwa kwenye maombolezo ya siku tatu, maana ndio sheria ya dini, msiba ni siku tatu tu. Baada ya hapo basi tunatawanyika kwenda kujitafutia riziki.

Nawashukuru wale wote walio onyesha nia dhati kabisa ya kutoa rambi rambi zao (Ubani) kwangu, Insha'allah Mwenyezi Mungu atawalipa kwa niya yako safi kwa kuonyesha kujali, binafsi sina cha kukulipa, zaidi ya kuwaombea dua na Insha'Allah Mwenyezi Mungu atawarahisishia mambo yao na kuwaepusha na mitihani ya kidunia.

Shukrani nyote.
 
pole sana mkuu mwache mama apumzike na yeye kwani hata sisi tutafuata kwani kila nafsi itaonja mauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…