Nimefiwa na mtoto jana muhimbili!

CHAI CHUNGU

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2012
Posts
7,113
Reaction score
933
Habari wana JF,nimefiwa na mtoto jana Muhimbili hospital.
Mazishi ni leo saa7 mchana,msiba upo banana ukonga!
 
Pole sana kwa kufiwa na mtoto wako bwana spika. Mungu akufariji na akupe nguvu.
 
Dah pole sana,mungu amlaze mahali pema peponi.amin.
 
Pole sana ndugu yangu,Mungu akupe faraja na nguvu.
 
kwa atakaye kua tayari kufika apige namba hii:0713 373132/0787 474142.
 
Bwana ametoa,Bwana ametwaa na Jina lake lihimidiwe.Ameni.
 
Pole sana,wewe na family yako,ningekuwa Dar ningekuja msiban,pole mno,Mungu akufariji.amen..n
 
pole sana mkuu.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina la Bwana libarikiwe amen! amen!
 
Pole sana Mkuu. Mungu akujalie nguvu ya kukabiliana na hali hii ngumu. naamini hapa sote tu pamoja nawe katika sala na maombi
 
Habari wana JF,nimefiwa na mtoto jana Muhimbili hospital.
Mazishi ni leo saa7 mchana,msiba upo banana ukonga!

Pole mkuu tumuombe mungu awape nguvu kwenye kipindi hiki kigumu cha msiba
 
Pole sana ndugu yetu. Mungu wa Israel na akupe faraja zake!
 
Pole sana mkuu, Mungu akupe nguvu na uvumilifu ktk kipindi hiki kigumu. Hakika sote ni wa Mungu na sote tutarejea kwake
 
Pole sana. Mungu na akawe mfariji wenu ktk kipindi hiki kigumu cha msiba.
 
Ni majaribu ambayo Muumba anatupitisha waja wake. Pole sana Spika. naamini Mungu atakujalia nguvu za kukabiliana na majonzi haya makubwa nasi tutaendelea kukuombea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…