Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Nimefuatilia mitandaoni nyendo za RPC Dodoma aliyeondolewa, nimefuatilia kuona mahusiano yake na jamii pamoja na utendaji kazi wake. Nachelea kuamini kwamba katika kinywa kile maneno yakumdhalilisha mwanammke aliyetekwa yanaweza kutoka.
Nimefuatilia mitandaoni hakuna sehemu kuna sauti inayosikika ya mwanamke huyu akisema maneno yaliyoripotiwa na vyombo vya habari vya mwananchi.
Lakini pia hakuna uthibitisho wowote uliotolewa na chombo husika kukanusha kauli yake kwamba HATA KAMA ANGEKUWA ANAJIUZA HAKUSTAHILI KUNYANYASWA.
Nimeona wanawake wengi wanamshambulia RPC kwamba ametenda kinyume cha maadili. Naomba niseme aliyekwenda kinyume cha maadili ni mwandishi wa habari. Tukiruhusu waandishi wa habari waandike wanavyotaka wao bila kukemea ipo siku itatoka habari ya kisiasa yakutuhumu mwanasiasa jambo ambalo hana uelewa nalo na tutakosa nguvu ya kukemea au kutafuta ukweli.
Viongozi watetezi wa haki za binadamu na mashirika mengine tuleteeni clip inayoonyesha haya mnayoyapinga ni kweli yamezungumzwa na muhusika.
Kesi hii ina interest kubwa ya jamii na kila mtu anatafuta namna ya kuvuruga kesi husika. Leo watu wamedanganywa nao wamehamia kwenye mjadala wakupambana na RPC ambaye ni mpambanaji wa haki za binadamu.
Upo uwezekano pia kwamba baada ya yeye kutaka watuhumiwa wafikishwe mahakamani labda wapo watu waliona siyo muda muafaka. Au yawezekana alipinga maamuzi flani ikabidi iwekewe zengwe.
Utaona hata baada ya RPC kuondoka chombo hicho kiliripoti kwa herufi kubwa MALAYA AMWONDOA RPC.....
Mimi natoa pole kwa huyu mama kwa magumu anayopitia lakini nitabaki kuamini huyu ni POlisi mcha Mungu, mpigania haki za wanawake toka akiwa Songwe na Mpenda haki.