Nimefungiwa pombe kwenye karatasi lenye taarifa za wachangia damu

Nimefungiwa pombe kwenye karatasi lenye taarifa za wachangia damu

pombe kali

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2014
Posts
282
Reaction score
561
Salamu, basi jana nikaona nichukue pombe kali nikanywee nyumbani, yule muuzaji akaniwekea kwenye bahasha nyeupe yenye maandishi pande zote.

Nilipofika nyumbani nikapiga fundo la kwanza na la pili kisha nikaanza kuipitia ile bahasha nilishtuka kidogo maana ina taarifa za wachangia damu wawili ikiwa na majina kamili, umri, anuani ya makazi.

Namba za simu hali ya afya ikiwa ana maambukizi ya magonjwa ya zinaa, ikiwa amewahi kufanya ngono kwa njia ya haja kubwa, au kwa njia ya mdomo....kweli hapa wizara ya afya mmetuangusha, utaratibu wa faragha ya wapatiwa huduma ukoje? ama utaratibu wa kuharibu nyaraka (disposal plan/policy) ni upi?

Bado naangalia kama itakuwa ni vyema hizo fomu nikiziweka humu ingawa kuna baadhi ya sehemu nitazificha ila pale chini kwenye jina la Afisa mtoa huduma na sahihi yake nitaomba nipaache kama palivyo... utu wa mtu uheshimiwe
 
Sababu ya 2,546 kupenda kunywea bia Bar.
 
Hatari sana juzi juzi nimechangia damu anyway hata hivyo nitaendelea kuchangia
 
Hatari sana juzi juzi nimechangia damu anyway hata hivyo nitaendelea kuchangia
Kabla ya kuchangia damu hakikisha una damu ya ziada, si kila mtu anatakiwa kuchangia damu hizi hospital za kawaida hawawezi kukwambia wao wanagema tu.

Niliacha kuchangia damu baada ya kuchekiwa kwenye maabara ya ukweli na kuambiwa damu niliyonayo inanitosha siyo ya kuchangia, niko negative maana JF hawachelewi kujitungia habari.
 
Back
Top Bottom