Nimefungua duka, nipeni ujanja wa kutoboa kwa kuwa Mangi

USIMAMIZI: Nimeona picha duka lako kwa kuanza ni zuri, siyo lazima uanze na mtaji mkubwa sana ingawa pia mtaji mkubwa ni kigezo muhimu cha kupata mafanikio ya haraka kwenye biashara ya duka. Pointi yangu muhimu ni kwenye usimamizi wa duka linaloanza kama hili la kwako, kina Mangi wengi unaowaona wakifakikiwa katika biashara za maduka si kama wanakwenda kwa sangoma (waganga) hapana, siri yao kubwa ipo katika usimaimiaji. Komaa hapo dukani mwenyewe ujue kila shilingi inayoingia na inayotoka.

Ukichanganya na ubahili kama member mmoja alivyokushauri hapo juu mtaji utakua haraka na mafanikio utayaona tu. Siri mojawapo nyingine ya duka baada ya usimamizi thabiti ni mtaji, duka likishakuwa na mtaji mkubwa ukiwa na kila bidhaa ni basi, hakuna mshindani ataweza kukubabaisha na ndipo kila mtu sasa ataanza kusema sijui ooo, umeenda kwa mganga sijui nini na mambo kama hayo.
 
waliouliza nauzaje 24 hrs nipo na rafiki yangu ambaye namuamiji sana tunapokezana sasa hv saa 9 zamu yangu hadi saa 6 mchana
 
Ongeza na miamala (anza na TigoPesa na Airtelmoney kama upo Dar),vocha na sigara zisikauke hapo. Mara nyingi hivyo vitu huvutia wateja wa bidhaa nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…