Binafsi, kutokana na uzoefu nilionao nina mambo kadhaa juu ya suala hili,
1. Kwanza siamini kama kweli hili jambo limetokea kwako, hii ni kutokana na reaction yako ilivyo ya 'kitoto' unless huyo binti ni girlfriend wako tu.
2. Hizi hoja za kwamba ooh labda humridhishi mkeo sidhani kwamba zinajibu kikamilifu hoja ya kwa nini wanawake wanatoka nje ya ndoa! Kisaikolojia, hamasa ya mapenzi kwa wawili huwa juu sana wanapoanza mapenzi, kadiri siku na miaka inavyoenda hii hamasa hupungua mpaka kufikia hatua mpenzi wako hata akiwa mtupu kabisa hushituki kwa lolote. Hii upelekea wote wawili kupunguza makeke katika mapenzi yenu. Hapa ndipo wengi wanapoanza kutoka nje taratibu kutafuta hamasa mpya.
3. Inapofikia hatua hiyo ya pili, BUSARA na MALEZI ya mtu katika mapenzi ni ya muhimu zaidi kuliko hata mapenzi yenyewe katika kuamua kwamba wewe utabaki kuwa na mke/mume wako mpaka kufa bila ku cheat wala nini!!
4. Katika mazingira kama hayo, maudhi yoyote ndani ya ndoa (hata kama ni madogo kiasi gani) hupelekea mume/mke kuanza ku cheat kidogo kidogo.
5. Unapogundua mkeo/mumeo ana cheat, uamuzi wako unategemeana sana na mambo yafuatayo;
-hatua miliyofikia kwenye ndoa yenu (mko kwenye 20's or 30's or 40's or 50's (i.e. stage in marriage life cycle). Wanandoa walio na umri wa 20-39 ni rahisi zaidi kuchukua maamuzi ya ku divorce kuliko walioko kwenye 40-60 n.k
-financial stability ya kila mwanandoa separately (individually)
-Idadi ya watoto mlionao na umri wao
-Sociol status yenu na ya wazazi wa pande mbili (kama mko nao kwenye mji mmoja)
-n.k
Kwa hiyo bwana NgomaNzito, kabla ya mtu kukushauri anahitaji kujua vitu hivyo hapo juu kuhusu wewe na mkeo!!