Nimegundua demokrasia haikuundwa kwa ajili ya Mwafrika

Nimegundua demokrasia haikuundwa kwa ajili ya Mwafrika

Eli Cohen

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
4,460
Reaction score
13,715
Mtu mweusi ni mkaidi sana.

Mpe uhuru, ajipatie nafasi ya kubania wengine uhuru.

Mpe mamlaka, ajipatie nafasi ya kutajirika haraka.

Mwafrika katika harakati analalamika kuhusu njaa na tabu, akipata ugali, anawaita wenye njaa ni washamba na wavivu.

Mwafrika hugeuza cheo kuwa kampuni, Mwafrika kwenda ofisini ni sawa sawa na barrick kwenda mgodini, ukijaribu kumtoa kwenye reli, kesho msibani unaimbiwa kwaheri.

Maana ya utawala kwa mtu mweusi sio uwajibikaji na utimizaji, maana ya utawala kwa mtu mweusi ni ulaji na kujimwambafai.

Siku njema mwafrika mwenzangu.
 
Back
Top Bottom