Nkulu wa nchito
JF-Expert Member
- Dec 13, 2019
- 2,078
- 2,759
- Thread starter
-
- #21
Vijana mnapata moyo wap mgumu kiasi icho mtu anakili na kutaka asamehewe na bado unasame
Mm haijaisha kwangu namlia timingVijana mnapata moyo wap mgumu kiasi icho mtu anakili na kutaka asamehewe na bado unasamehe
😀😀😀Mnaooa halafu mnanyimwa tendo mna akili za ajabu sana.
Ukiona anakunyima wewe wali ujue kuna mtu ametoka kujipakulia pilau ndio maana anahofia utasikia harufu ya pilau. Siongelei wali na pilau hapa
Inawezekana kabisa siyo uongoMkabidhi kwa mama yake kwa amani. Miaka yote hiyo yuko mbali na wewe, inawezekana hata hao watoto au mmoja sio wako. Think
Unasubiri nini kukata hiyo kamba ?Wakuu habarini za siku nyingi, poleni sana kwa yaliyotokea.
Kijana mwenzenu nilifunga ndoa mwaka 2021, lakini kutokana na mambo ya ajira mimi na mke wangu tunaishi mbali mbali. Hapo mwanzo sikuona changamoto yoyote, lakini baada ya miezi kama mitatu nikaanza kuona utofauti.
Ukipiga simu usiku utakuta iko busy, nikamuuliza kwa nini simu yako inakua busy usiku, akaniambia labda ni mtandao. Pia wakati mwingine akipokea simu huwa anaweka mlio wa chini sana, kiasi kwamba huwezi hata kusikia ikiita.
Wakati mwingine anaifunika, yaani hata ukipiga huoni kama inaingia. Hapo ndipo nilipoanza kupata wasiwasi, kwanini inakuwa hivyo.
Siku moja nilikuta namba mbili za simu kwake, nikazichukua zote nikazihifadhi kwenye simu yangu. Baadaye simu yangu iliharibika, nikatoa laini yangu nikaweka kwenye simu ya mke wangu ili niende kununua nyingine.
Sikujua kuwa moja ya zile namba nilizochukua kwake ilikuwa imetuma ujumbe kwenye laini yake, na jina likajitokeza lile nililosave. Aliposhtuka, akaniuliza, nikamwambia sijui.
Lakini mtu mwenye akili angejua kabisa pale taa ya kijani ilikuwa imeshawaka.
Siku zikapita, wakati fulani alikuwa likizoni na tulikuwa nyumbani wote. Simu yake aliiacha sebuleni wakati yuko jikoni anapika. Simu ikaita, kama kawaida haina mlio. Nikaangalia, nikakuta ni ile namba niliyosave. Nikapokea ili nijue ni nani.
Niliposikia sauti, ilikuwa ya mwanaume, anasema “halloo.” Mimi nikanyamaza nikasepa kidogo. Niliporudi nikamuuliza, “ile namba uliyoniambia ni mdada, mbona sauti ya kiume?” Akanyamaza kimya.
Nikamwambia apige tena. Alipopiga, yule jamaa aliposikia sauti yangu hakusema chochote, akajifanya kama hasikii, kisha akakata. Nilipiga tena mara kadhaa lakini hakupokea.
Nikamwambia mke wangu anipe PIN ya simu yake, akanipa. Nikachukua simu yake na ile ya beki tatu nikaondoka nazo. Ilikuwa Ijumaa.
Nilikaa nazo hadi Jumatatu niliporudi nyumbani. Jumapili, alitafuta simu sijui ya nani akanipigia, akaniomba nirudi nyumbani tuongee. Sikurudi.
Niliporudi Jumatatu asubuhi, nilimpigia mama yake simu, nikamueleza yote yaliyotokea. Nilifanya hivyo kutoa tahadhari tu, nisije nikasikia mambo mengine huko mbele. Mama yake akaniambia ataongea naye, lakini najua wamama na watoto wao wa kike mara nyingi hufichiana siri. Nakumbuka tukio kama hili liliwahi kutokea kwa mwandishi mmoja wa ITV.
Jioni niliporudi nyumbani, mke wangu akaomba msamaha. Lakini picha ilikuwa wazi kabisa, kuna usaliti. Nilipokuwa nimeishikilia simu yake, nilikuta amenificha asiweze kuona status zake anazopost.
Nilipoangalia kwenye orodha ya waliompigia simu, nikaona ile namba pia huwa inampigia usiku.
Nimejitahidi sana, nimekaa muda mrefu bila kumtongoza msichana yeyote, lakini mwenzangu hanielewi.
Kuna kipindi alikuwa hataki hata kufanya tendo la ndoa, akisema anatumia njia ya uzazi wa mpango. Kwa jinsi mambo yalivyo, naona kabisa ndoa hii haitofika mbali.
Imebaki kushikiliwa na kipande kidogo cha kamba, muda wowote inaweza kukatika.
Moto nampelekea kusema kweliAcheni kuwadinya wake zenu kimazoea,,,
Polee sanaa mkuuKwanza haja cheat sababu yako, Dawa pekee ya msaliti, ni kujiondoa bila ugomvi bila kuwaza gharama, nimesamehe mke wangu mara 2 kwa usaliti, akarudia ya 3, najuta kwa Nini nilimsamhe na kukaa kwenye ndoa kwa Miaka 15 na yakarudia, ondoka mdogo wangu, ondoka, utafanikiwa hata kama sasa huoni njia
Hakuna mbinu inayoweza kuwa guarantee kwako ili uweze kupata mwenza muaminifu, mtu mwenye hulka ya usaliti siku zote atairudia tabia yake hata umpe nini ndo maana wimbo wa usaliti upo kwa matajiri na masikini.
Isipokua malezi ya mtu, iman yake , hulka yake , ustaarabu wa familia aliyotoka , mapenzi yake ya dhati kwako inaweza kumfanya aheshimu utu wake na awe muaminifu kwako.
Usiangalie tu sijui nimuoe kwasababu ana kazi tusaidiane maisha, unaweza ukamuoa na asikusaidie na moto ukauona vilevile, na kwanza lengo la msingi la ndoa siyo hilo, lakini pia hutakiwi kukaa mbali na mke wako labda iwe tu kwaajili ya safari au masomo ila siyo kikazi, kama kazi inakufanya ukae mbali na mke wako labda kwakua nae kaajiriwa sehemu nyingine hapo lengo la ndoa linakua halina maana kabisa.
We ni bonge la Lofa,fala wewe unamfwatiliaje mwanamke wa watu namna hiyo.
Si ungepoteza huo muda kutafuta hela.
Yaani uko tu nyumbani umeshika simu za wanawake unasoma mesage zao
Nashukuru sana kwa ushauri wakoBro CHIN. ✊✊✊
Naomba asome haya uliyoyaandika kwa umakini.
Na sio yeye tu. Wanaume wote inatuhusu.
Wanawake wanaochepuka sio kwasababu mwanaume wake hampi hili au lile.
Ila kwasababu ya tabia na hulka ya mwanamke.
Kuna mdogo wangu wa Hiari . Anafanya kaz Benk. Ana watoto wawili kwa ndoa mbil tofaut za Kiislaam.
Ashaolewa mara 3. Na zote wametengana.
Sasahiv amepanga anaishi mwenyewe . Watoto kwa bibi.
Ila yote hii ni ili awe na uhuru wa kutoka na kunywa bia (anapenda sana starehe na outings) . Na akilewa zinashuka chini. Wana wanajipigia vya kutosha.
Kwahiyo ndo 3 zote naweza kusema tatizo ni mwanamke na sio hao wanaume.
Nkulu wa nchito pole bro.
Ila ipo haja ya kuchunguza je mkeo hiyo ni tabia yake alikuwa nayo kabla hujamuoa?. Anayewasiliana nae ni X wake?. Hao watoto wanafanana na ww au yeye(kama hawafanani na mmoja kati yenu . Chunguza).
All in all. Jipe Muda. Usikurupuke kumuacha kabla ya kuchunguza zaidi.
Huu ndo ukweli ijapokuwa wabishi ni wengiiiDemu aliepita chuo kusaliti ni kama kunywa maji,wengi nawaona watumishi wa kike hawajali kabisa
Kosa lako la kwqnza ni hiliKijana mwenzenu nilifunga ndoa mwaka 2021, lakini kutokana na mambo ya ajira mimi na mke wangu tunaishi mbali mbali