comte
JF-Expert Member
- Dec 11, 2011
- 9,019
- 6,825
Kwenye Taifa lenye zaidi ya 80% ya watu wake wakiwa na umri chini ya miaka 35, ni dhamira yetu, kuwekeza na kutengeza sera, sheria na taratibu zitakazohakikisha kuwa vijana wa taifa hili wanakuwa kipaumbele na chachu ya maendeleo, kwao wao na kwa taifa.
Serikali ya ACT-Wazalendo, imekataa kuona vijana wa taifa hili wananyang’anywa fursa, wanakatishwa ndoto zao, wanakandamizwa na kufanywa watwana ndani ya taifa lao. Serikali itakayoundwa na ACT-Wazelendo, itakuwa Serikali ya vijana kwa ajili ya vijana wa Tanzania wa kike na wa kiume.
Lakini pia itakuwa Serikali ya kuandaa na kusimamia upatikanaji wa maisha stahiki uzeeni kwa kuwa na mfumo madhubuti wa Hifadhi ya Jamii ambao utahakikisha kuwa kila Mtanzania anakuwa na Bima ya Afya na Pensheni akifika umri wa kutoweza kufanya kazi. (Ilani ya uchaguzi ACT WAZALENDO 2020-2025: iv)