Nimehakikisha sipo peke yangu, haupo peke yako

Nimehakikisha sipo peke yangu, haupo peke yako

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Natumai mmeamka salama kwa Neema na Baraka za Mungu. Tumshukuru Mungu sote kila moja kwa namna yake, kwa kibali na zawadi ya Uhai na Afya alizotukirimia tena leo.

Nikiwa naelekea kwenye mishemishe zangu na labda baadae kidogo kwenye ibada ya pili, mitaa ya Mwenge. Nimepata fursa ya kusikiliza wimbo wa gospel unaitwa SIPO PEKEYANGU NIKO NA MUNGU. Nimebarikiwa sana, na ghafla nikakukumbuka wewe rafiki, ndugu, jamaa, kiongozi na mwana Familia na member wa JF.

Kwa Imani na upendo wangu kidogo sana, naamini hauko peke yako pia katika mahangaiko, mipango na shughuli zako za kila siku. Upo na Mungu mwenyewe na halisi kabisa. Hata wewe unaeelekea kanisani hauko pekeyako, upo na Mungu na unaelekea kumtukuza Mungu, hongera sana na ubarikiwe sana.

Amenihakikishia mimi na nina hakika ameambatana nawe sasa, daima na Milele.

Hebu barikiwa zaid na wimbo huo niliouambatanisha hapo chini na Mungu akubariki sana.

Nakutakia Jumapili Njema Sana, wewe na Familia yako.

Kula chuma hiko...
 

Attachments

Back
Top Bottom