Nimehukumiwa kulipa pesa, sina uwezo

MIGNON

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2009
Posts
4,108
Reaction score
5,110
Wadau naomba msaada wa kisheria.

Nimehukumiwa nimlipe mshtaki wangu milioni sita wakati kazi sina na wal sina asset yoyote ninayoweza kuuza ili kupata pesa hiyo.Itakuwaje?
 
Kwa kosa lipi? Mi sio mtaalamu wa sheria ila nadhani unaweza kukata rufaa kama hujaridhika na hukumu, kama umeridhika nayo basi inabidi ulipe
 
Hakuna sheria inayokulazimisha kulipa ikiwa huna uwezo, au kulipa kwa kiwango cha juu ya uwezo wako. Lakini ujue pia uwezo ni kutia ndani mali unazomiliki. Hivyo unaweza kunyanganywa gari lako, nyumba nk vilivo katika jina lako ili vipigwe mnada kulipia deni.

Sasa kutokuwa na uwezo au kazi sio kisingizio cha kukwepa deni. Ikiwa anayekudai ataithibitishia mahakama kwamba una uwezo wa kulipa, mfano kutokana na mali ulizonazo, basi utaamuriwa ulipe. Ikiwa wewe una uwezo wa kuthibitisha huna uwezo wa kulipa deni, unaweza kuiomba mahakama ulilipe deni ndani ya uwezo uliothibitishwa ulio nao; mfano Tshs 1000 kwa mwezi, hata kama hilo deni ni la Tshs 10M.

Kikubwa ni kwamba anayekukopesha pesa anapaswa kuhakikisha una uwezo wa kulipa deni kabla hajakukopesha. Sasa isije pia ukawa ulidanganya juu ya uwezo wako wa kulipa wakati wa kukopa, kwa sababu, japo deni halipaswi kumfunga mtu jela, kama ulidanganya juu ya uwezo wako itakufanya ufunguliwe criminal case - utapeli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…