"Walimu kama mnaona mshahara huu tunaowalipa hautoshi acheni kazi hii na nendeni kutafua kazi ingine"Nanmkuru mama Mwantumu Mahiza akiwaambia walimu wa serikali ya Muungnano wa TZ alipokuwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Mtwara/Lindi mwaka jana!
Kama Mama huyu kwa kauli hii angekuwa anagombea kwenye jimbo la watu wenye msimamo mikali kama vile Mtera(Dodoma),Kyela(Mbeya)hata jimbo lolote lililopo ZNZ hasa Pemba siku ile ya kuchukua fomu angekutana na wananchi wenye hasira nje ya ofisi za CCM na kumtaka ili kutuliza hasira zao aichane pale pale fomu ya kugombea aliyoichukua!
Kumuachia hadi kushindwa na Danstan Kitandula ni udhaifu ungine waliouonyesha wana Tanga;kauli ya kukera na hovyohovyo kama ile bado anajaribu hata kushika nafasi ya pili?Huyu alistahili akose hata sifa ya kuchukua fomu;"wazee"walitakiwa watumwe kumuambia kuwa hata fomu hatakiwi kuchukua maana ataleta mpasuka mkubwa ndani ya CCM wilayani, wananchi wasio wafuasi wa CCM na familia za walimu alio wasimanga!
Mama Mahiza;kazi zipo nyingi tu mbona,kazi sio tu lzm uwe mbunge!