Nitajulikana
JF-Expert Member
- Sep 20, 2017
- 328
- 355
1.Japo wengine walalama,Huku wengine wasifu,
Serikali imesimama,Japo si takatifu,
Maendeleo kuleta,Sio kazi ya kubeza,
Serikali ya wanyonge,Wanyonge waneemeka?!
2.Madudedude twaona,Twasema maendeleo,
Bombadia kupishana,Reli ndo wimbo wa leo,
Bomba mafuta kufana,Hakika ni mamboleo,
Serikali ya wanyonge,Mifuko yao kumbuka.
3.Wengi kwa kweli walia,Huku sifa wakimwaga,
Wachache washangilia,Kuku na keki kumwaga,
Akili zao waficha,Kuiona kesho yao,
Serikali ya wanyonge,Mpe uhuru Mnyonge.
4.Mkute tu hadharani,Malaika wetu kafika,
Mkute kwake gizani,Kiama kimetufika,
Mpe nafasi aseme,Ujue wake msingi,
Serikali ya wanyonge, Msikilize Mnyonge.
5.Nyumba na baba salama,Wapambe ni shangilio,
Baba vikwazo ni hima,Kuepuka shambulio,
Mashindano kukimbia,Mbio za mita mia,
Ashike aache lipi,Mnyonge aachwa solemba.
6.Bi keafu,wochi iti,Watoa ubuyu watishwa,
Wakalia moto Kiti,Madhaifu yakishushwa,
Twajua so Malaika,Changamoto kuepuka,
Wanyonge nao wajua,Wape nafasi wanene.
7.Kahawa korosho pamba,Mnyonge hana majibu,
Taharuki kumkumba,Maisha kwenda kibubu,
"Hapa ni kazi" twasema,Mjasiri Mali kuhema,
Wapambe tonya mzee,Huku tuliko ni jela.
8.Ndugu zangu watumishi,Eti nyinyi ni vigori ?
Nidhamu kazi kuiishi,Maisha kuwa shubiri,
Chifu wakumbuke hawa,Ufanisi kazi ujiri,
Serikali ya wanyonge,Mnyonge ni nani hasa?
9.Elimu eti ni bure,Imekubali matakwa ?
Tena ajira bwerere,Wahitimu kurundikwa,
Vijana ipi mipango,Maisha yao kuponywa,
Mnyonge ndani ya giza,Mpeni mwanga jamani.
10.Wapambe tuelekeze,Ni wapi twaelekea,
Matumaini tujaze,Kesho ya kusherekea,
Kubana yenu agenda,Mwavuruga mstari,
Mjuze kesho wanyonge,Aunge mkono juhudi.
Sent using Jamii Forums mobile app