Elections 2015 Nimeipenda hii ya Mwigamba kwa Mwanakijiji

kuna tatizo moja la CDM kudhani kila kitu kipo sawa kama wanavyotaka wao, hujuma wanazijua walishinda Igunga sasa walishindaje wasishinde Igunga na leo Arumeru? Hii ndiyo hoja ya Mwanakijiji.
 
Kwa Muda nimekuwa nikipitia Hoja za Mwanakijiji ndani Na nje ya Jamvi hili.. Hata Hoja yako unayomchambua mwigaz hapa nimeisoma Kwa makini. Sasa nashawishika kufikiria kuna agenda ya Siri ndani ya matamshi Na maandishi yako ambayo hutaki kuiweka bayana.
Majuzi tulibishana sana juu ya Mabadiliko juu ya maandiko ya Mwanakijiji. Wengine walisema ameshamezwa Na Gambaz wengine walisema ni Bomu la Mtu. si Lengo langu kukunanga Nguli wa habari kama wewe kwamba umeshachakachuliwa au si Lengo langu kukushinikiza kuandika mema ya Chama fulani Na Mabaya ya serikali Na cha Chake la-hasha, Lakini maandiko yako ya siku hizi za usoni yamepoteza mvuto wa uhalisia Wa Mwandishi mahiri. Ni kana kwamba kuna Nguvu ( nje Na Utashi wa asili yako) unayokushurutisha kuandika unachoshurutishwa kuandika Kwa mantiki ya kuibua hisia ngeni Kwa wasomaji wanaopenda nakala zako. Mathalan niliposoma andiko lako CHADEMA wakipoteza jimbo (Arumeru Mashariki ) Basi Timu nzima ya Uongozi wa juu (ambao hukuutaja Kama ni wa kitaifa au la) unapaswa Kujiuzulu. Kwangu nilisoma Kwa matarajio kadhaa, kwanza kujua kwanini umeoanisha uchaguzi wa jimbo Na viongozi Hao uliowaita wewe ambapo sikupata jibu, pili kwanini ulienda mbali Kwa kuwataka wajiuzulu Na si vinginevyo ambapo pia sikupata jibu ila top nilitarajia Basi utawataka wajiuzulu kisha utoe pendekezo mbadala Lakini hujafanya hivyo.. Ukasema tu wajiuzulu enhe kisha?!! Nani awe nani baada ya hayo.. Maandiko ambayo Hayana majibu yanalenga kuchanganya jamii Na sio uandishi mzuri Kwa Nguli wa tasnia hii Kama wewe. Mwigaz katika Kurunzi lake hili amepambanua kwenye dhima ya andiko lake kwamba Ziko sababu kadhaa si kura tu inayoweza kufanya mtoa tangazo aka tamka ushindi Kwa mgombea. Akasema kuna Kura ya mwananchi, nguvu za Dola akimaanisha Tume, Serikali, Polisi, Usalama wa T, Lakini pia kuna Mabavu, sasa Katika mchango wa majibu yako umekuwa mbishi tu, ukinukuu vifungu vyake Na kuvikosoa Na kusahau dhima ya awali ya andiko lako kuhusu kujiuzulu Kwa viongozi uliowataka jimbo wasipolinyakua.
Ndiposa Narejea kwenye wasiwasi wangu kwamba si bure Mwanakijiji naye "ameshatembelewa" Na "akatembeleka".. Kama ni kweli Basi itakuwa aibu sana kwenye utashi Wa nafsi yako Kama mzalendo..
 

:focus::focus::focus:
 
kuna mambo inawezekana sijayasoma from MMM au kuelewa from others.... kushinda Arumeru kunawezekana, ila itakua ni kujenga nyumba kwa tofali la baragu kwani madiwani wana role kubwa ya kuplay

I may be off topic but i think Mwigamba and MMM all missed something....... the power of ignorance!!!
 
Yamekuwa haya tena!
 

Mkuu swala la kufanya library research mwisho wake unaishia kuandika hadithi za kusadikika.
Hii ni moja Kati ya maandiko yaliyo-shake credibility ya weledi wako mzee.
Hujioni kama unalazimisha kushindana while unapaswa kujibu hoja za msingi hususani kutoka kwa mtu anayefanya field research.
Unaposingizia kuwa eti mwigamba kasema CDM wataandamana hata wakitangazwa sio washindi kihalali unadhihirisha kuwa unajilazimisha kutokuelewa hili hali unajua hicho ulichokisema hakijaandikwa wala kusemwa ktk makala hii ya mwigamba.
Mpaka sasa siamini kama haya unayoandika unakusudia au ni tatizo la kujivua ufahamu hasa ukizingatia huendi kwenye field.
Naamini ungeonyesha busara kwa kukiri kuwa si sahihi kuzungumzia maswala makubwa pasi kufanya research za maana(hasa field research).
Muungwana angefurahi kusahihishwa ili aweze kufanya kazi nzuri zaidi hapo baadaye.
Kubali hii ni challenge, ulichemka mzee.
 

Well, nasimamia kila neno nililoandika. Na 'field research' hakuna aliyefanya unless neno 'field research' limepoteza maana. Haiitaji mtu kuwa on the field kujua kinachoendelea kwenye sehemu hiyo kuna njia nyingi tu za kujua.
 
Makala za Mwanakikjiji zinahitaji tafakuri kubwa,sidhani kujiuzulu anakomaanisha kwa viongozi wa chadema,ni kujiengua na kukaa pembeni.Nakumbuka maneno aliyotamka F.Mbowe wakati wa ufunguzi wa kampeni Arumeru.Alisema''Serikali ya CCM ina polisi,jeshi mgambo na kila kitu,ila CHADEMA ina nguvu ya umma''.Inatosha tu kusema juhudi za viongozi wa CHADEMA katika hili zinaonekana wazi,hivyo basi kama ni kuwajibika,wawjibike Wananchi wasiyoyaelewa mabadiliko,wawajibike Maafisa wa tume watakaopindisha matokeo ,na viwajibishwe vyombo vya usalama ambavyo vitashindwa kutenda haki na usawa.
 


Hapa kwenye kutumia busara ndipo MM unapotofautiana sana na wapenzi wengi wa CDM
Hata pale wanaposhindwa kwa haki wao hukimbilia kusema wameshinda na kutaka kuleta vurugu.Huu sio utu na ustaarabu na dhana nzima ya kupiga kura inatoweka.
Binafsi nimeshakutana na wanachama wengi wa CDM ambao wao ni siasa ya ushindani inawashinda na kutangaza vita hapa pale panapostahili mazungumzo.
Tabia hizi ndizo zinairudisha CDM nyuma na ni wachache sana wanaoliona hili na kulifanyia kazi.
Ukishindwa kubali na mpongeze aliekushinda.
Hata wananchi wataona kuwa CDM ni chama komavu.
OTIS
 
Well, nasimamia kila neno nililoandika. Na 'field research' hakuna aliyefanya unless neno 'field research' limepoteza maana. Haiitaji mtu kuwa on the field kujua kinachoendelea kwenye sehemu hiyo kuna njia nyingi tu za kujua.

Nimekupenda, una uelewa mzuri sana. Unajua, Mwigamba kuwepo kwake Arumeru basi anadhani anaelewa mambo ya hapo kuliko mtu aliyeko mbali na huko. Kwanza naamini hata makala yake ni ya kutaka kujenga hoja kwamba CDM watashinda wakati hata moyoni mwake hana uhakika huo. Mimi nilikuelewa sana ulipotumia neno "kujiuzulu" ulikuwa una maana gani. Najua hata yeye ni kiongozi wa CDM Arusha ndiyo maana imemchoma sana ile makala yako. Anyway ninachotaka kusema hapa Mwigamba namkubali kwamba ni mwandishi mzuri, lakini naye ana dosari, kama mimi, Mwkjj na mtu mwingine yeyote. Mimi naamini Mwigamba hayupo rational, yeye ni irrational kwani anataka watu wamwamini yeye tu hata pale yeye mwenyewe toka moyoni mwake hana kile ambacho anataka watu wengine waamini toka kwake.
 
cccm mchezo mchafu acheni jamani. tuachie arumeru yetu salama
 
Huyu nguli yupo wapi siku hizi?
 
Haya maneno yameishihadi sasa, uliandika tarehe 28/3/2012 ni miaka 7 iliopita, was like prophecy na imetokea kweli kwamba MMM alikua na ajenda ya siri since that time. Bahati mbaya hata Mwigamba na yeye kapotea kabisa, sio kwenye siasa tu bali hata kwenye uandishi, haonekani!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…