Elections 2010 Nimeipenda sana hii.

Mlachake

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2009
Posts
4,437
Reaction score
4,618
Kwa hisani ya Francis Godwin.




NI NANI KATI YA HAWA UTAMPIGIA KURA YAKO OCTOBA 31 ILI ATIMIZE AHADI ZAKE KAMA RAIS WAKO? TUJITOKEZE KWA WIKI KUCHAGUE ,RAIS,MBUNGE NA DIWANI


Dk Mohammed Shein (CCM)
1) Kuboresha maisha ya wavuvi-Chakechake Pemba
2) Kusomesha wafanyakazi-Mnazi mmoja
3) Kipaumbele katika elimu -Unguja na Pemba
4) Kipaumbele katika afya-Makombeni Mkoa wa Kusini Pemba.
5) Kuulinda Muungano- Wawi kisiwani Pemba
6)Kuleta mabadiliko Zanzibar-Pemba na Unguja
7)Kuboresha Bandari ya Zanzibar kwa kuijenga upya-Kibandamaiti
8)Kuboresha Maendeleo Zanzibar- Jimbo la Wete, Pemba
9.Ujenzi wa maktaba kubwa na nzuri Kisiwani Pemba- Mtambwe
10.Kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu Zanzibar- Kijiji cha Kambini Mchangamdogo
11.Kuimarisha miundombinu Kisiwa cha Pemba- Kijiji cha Makombeni Mkoa wa Kusini Pemba
12.Kuhamasisha wawekezaji kuwekeza Pemba katika miradi mbalimbali-Makombeni Mkoa wa Kusini Pemba.
13.Ahadi eneo la Micheweni kuwa maeneo huru ya uchumi- Micheweni Kaskakzini Pemba
14. Kumaliza matatizo ya maji mkoani -Mkoani
15..Kujenga Bandari ya kisasa katika eneo la Mpiga Duri Unguja- Mkoani
16.Kuiamrisha makazi bora kwa Wazanzibar- Mkoani

Ahadi za Profesa Lipumba na Maalimu Seif(CUF)
1.Elimu ya bure kuanzia msingi hadi chuo kikuu
2.Kubana matumizi kwa kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri
3.Kuunda serikali shirikishi
4.Kusimamia rasilimali
5.Kuimarisha miundombinu
6. Kusimamia na kuboresha afya
7. Kuboresha kilimo, viwanda na uwekezaji
8. Kurudisha chakula cha bure mahospitalini

Ahadi za Dk Slaa(CHADEMA)
1.Kujenga nchi isiyo na ufisadi
2.Kufufua Tanganyika ili irejee mezani kujadili muungano na Zanzibar
3.Kufufua uchumi wa nchi kwa kutumia rasilimali zilizopo
4.Kukata asilimia 20 ya mshahara wa rais
5.Kupunguza mishahara ya wabunge kwa asilimia 15
6. Kuweka Mwenge wa Uhuru Jumba la Makumbusho
7. Kutoa huduma bora za afya bure
8. kufuta kodi ya vifaa vya ujenzi
9. Kuwalipa wazee wa EAC fedha zao ndani ya siku 100
10. Kubana matuzi Ikula (Yuko tayari kula mihogo


Maalimu Seif Sharif Hamad(CUF)

1. Zanzibar kuwa kama Hong Kong – Unguja
2.Kuendeleza mashamba ya Karume- Kibanda maiti
3. Kubadilisha katiba na kuunda katiba mpya ya muungano na Zanzibar- Pemba
4.Kubadilisha mfumo wa uteuzi makamishna wa tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC)- Unguja
5. Kuwaunganisha wazanzibari ili kujenga umoja, udugu na ushirikiano-Pemba
6. Kuwasilisha hoja ya kubadili katiba ya Zanzibar na ya Muungano-Viwanja vya Kibanda Maiti
7. Kuondoa bajeti ya ZEC isiwe chini ya waziri kiongozi na badala yake kuwa inajitegemea yenyewe- Pemba
8. Kuondoa ulazima wa mwenyekiti wa tume kuwa jaji na badala yake awe mtu anayejua sheria-Unguja
9. Serikali kuundwa na vyama vyote vilivyopata ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi- Unguja
10.Kujenga jamii yenye maelewano na umoja -Pemba
11.Kutokochagua kiongozi kwa urafiki bali kwa uwajibikaji na uadilifu -Unguja na pemba
12.Kudhibiti vyombo vya dola vinavyofanya kazi kwa matakwa ya watu binafsi -Kibanda maiti
13.Kukomesha rushwa-Mkanyageni Mkoa wa Kusini Pemba
14.Kuhakikisha ununuzi wa zabuni unakuwa wazi na wananchi kuruhusiwa kuhoji kuhusu zabuni-Jimbo la ole Pemba
15.Kuongeza kima cha chini cha mshahara hadi Sh150,000-Mkanyageni Pemba
16.Kubadili vikosi vyote vya usalama na kulipwa mishahara kima cha chini kulipwa Sh180,000-Chakechake Pemba
17.Kubadilisha kikosi cha KMKM kuwa kikosi cha mwambao-Wawi
18.Wazee kupanda daladala bure na wale wasiokuwa na watoto kulelewa bure-Majimbo ya Chakechake
19.Kufuta michango yote ya shule za msingi na sekondari, kila mwanafunzi kuwa na kompyuta na badala ya kuishia darasa la saba sasa kuishia kidato cha sita-Hoteli ya Bwawani
20.Kutoa kitambulisho cha kila Uzanzibari na kufuta cha Mzanzibari mkaazi- Uwanja wa Hospitali ya Mnazi Mmoja
21.Kila mzanzibar kupata pasi ya kusafiria- Hoteli ya bwawani Zanzibar
22.Kuanzisha shirika la ndege Zanzibar -Viwanja vya Kibanda maiti
23.Kupandisha uchumi wa Zanzibar kutoka 6.8 hadi 15 kila mwaka kwa Zanzibar -Unguja
24.Kutoa uhuru zaidi kwa vyombo vya habari pamoja na kusaidia uanzishwaji wa Baraza la Habari Zanzibar-Unguja na Pemba
25. Kuweka hadharani nambari yake ya simu - Viwanja vya Kibanda miti
26. Kubadili sheria ya uwekezwaji-Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar
27.Kila mwanafunzi kuwa na komputa yake-Viwanja vya Kibanda maiti
28.Akiwa rais hata waziri au mkewe atafungwa akiwa ametenda kosa-Viwanja vya Tibirizi Kisiwani Pemba
29.Kujenga bandari ya Mkokoto na Pemba ili kuweka usafiri wa haraka wa boti ziendazo kasi-Tibirizi Kisiwani Pemba
30. Ahadi kudhibiti kuvuja kwa mitihani- Unguja

Ahadi za Kikwete(CCM)

1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora

  1. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
  2. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga
  3. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga
  4. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
  5. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
  6. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
  7. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
  8. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera
  9. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini
  10. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  11. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
  12. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
  13. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera
  14. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya
  15. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera
  16. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  17. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza
  18. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
  19. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
  20. Kulinda muungano kwa nguvu zote-Pemba
  21. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
  22. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini
  23. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
  24. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  25. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
  26. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
  27. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
  28. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
  29. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
  30. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
  31. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
  32. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
  33. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara
  34. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma
  35. Kulinda haki za walemavu- Makete
  36. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
  37. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
  38. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  39. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora
  40. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini
  41. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
  42. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  43. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini
  44. Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .
  45. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
  46. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  47. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
  48. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
  49. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
  50. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
  51. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa
  52. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
  53. kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
  54. kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo ,Iringa
  55. ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  56. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kabandamaiti mjini Zanzibar
  57. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
  58. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
  59. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
  60. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
  61. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
  62. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  63. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
  64. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
  65. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha
  66. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha
 
jk ni noma.Amemwaga Ahadi kama anaimba taarab.
 
jk ni noma.Amemwaga Ahadi kama anaimba taarab.Yaani utafikiri anatoa fedha zake mfukoni.Mambo mengine yanahitaji bunge kupitisha kwenye bajeti.
 
Huyu wa mwisho ni msanii tu...Hawezi kutimiza ahadi hizo zote, wakati majukumu ya kuendesha nchi yako palepale!
 
jk ni noma.Amemwaga Ahadi kama anaimba taarab.


kuwamwaga ahadi nyingi hakuna maana kushindwa kutimiza ahadi, vivyo hivyo kama ilivyo kwa ahadi chache. Kutimiza ahadi kunategemea ulivyojipanga na hasa kupenya kwenye mtandao wa wafadhili wa nje na ndani wanaosaidia uwezeshaji wa uchumi wa ndani. Hakuna serikali isiyokopa kwa ajili ya maendeleo yake. Jakaya kikwete hana shaka ataweza kazi hiyo.
 
Jamani hizo bajaji Dk wa Ukweli jana kasema zilishapitishwaga na bunge kitamboooo mpaka wakawa wanaziulizia. Ahadi nyingi za JK ni zile zilizopitishwa na bunge tayari na zipo kwenye mchakato.

Mfano majengo ya wamachinga ni mpango wa mfuko wa jamii NSSF wala sio wa JK
 
Ni kujidanganya kwamba mgombea akitoa ahadi chache ndiye atatimiza wajibu wake. Kutekeleza ahadi ni wajibu na dhamira ya dhati. utekelezaji haupimwi kwa wingi na uchache wa ahadi. Kwa mfano, tunaona wabunge na madiwani wana wajibu mdogo na ahadi chache kuliko za Rais lakini hawatekelezi ama wanatekeleza nusu wa walichotuahidi. Kikwete ana fursa nzuri ya kutimiza kuliko wagombea wengine
 
huyu kweli ni mwana mashairi hata angepewa miaka 20 ya kutawala hawezi kumaliza ahadi hizo,
wizi mtupu
 
Huyu wa mwisho ni msanii tu...Hawezi kutimiza ahadi hizo zote, wakati majukumu ya kuendesha nchi yako palepale!


Kinana kasema ahadi nyingine ni za kwake binafsi na wala si za chama
 
Rais Jakaya Mrisho kikwete ndiye mwenye dhamira ya kweli.
 
Kinana kasema ahadi nyingine ni za kwake binafsi na wala si za chama
na hii ni kwa sababu Kikwete ana uchungu na nchi hii hadi anatoa ahadi nje ya ahadi zilizomo kwenye ilani ya chama chake, ni marais wachache wanaoweza kuwa na vyanzo vyao vya fedha kwa ajili ya huduma kwa wananchi.
 

Kashindwa kutimiza ahadi chache za 2005, ataweza kutimiza ahadi lukuki za 2010? Hastahili tena kupewa ridhaa na Watanzania ya kutuongoza.
 
Kwangu mimi,
(1) Lipumba; Anaongelea sera zaidi which is good hata hivyo haonyeshi mikakati ya utekelezaji(Mipango)

(2) Slaa; Anaelekea hakuwa amejiandaa maana nyingi ya ahadi zake hazina serious impact kwa maisha ya mtanzania. Anazungumzia hatua zaidi kuliko sera au mipango.

(3) JK;Amekwenda down kwenye mipango na ndio maana ahadi zake zinaonekana kuwa nyingi na nimezistudy over 70% ni mipango ambayo ni on-going. that means they are practical.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…