Stephen Ngalya Chelu
JF-Expert Member
- Oct 31, 2017
- 8,252
- 18,335
Nina kasimu kadogo aina ya OKING (OK 1710) nilikokanunua kwa shilingi za kitanzania elfu kumi na nane tu (18,000/=). Kwa kweli kwa bei hii sikutarajia kupata simu yenye teknolojia ya hali ya juu kama hii.
Iko hivi, leo nilikachomeka chaji ili niende nacho kufanya mazoezi maana kina nyimbo ninazozisikiliza wakati wa kukimbia. Sasa baada kukitoa chaji nikaona ninaendelea kuonyesha kuwa kunapokea chaji. Nilishangazwa kwa kweli, nikadhani kuwa hali itakoma baada ya muda lakini kiliendelea kuingiza chaji.
Nimeenda uwanjani, nimefanya mazoezi, nimerudi, bado kinaingiza chaji na kinagonga mziki mwanzo mwisho. Hadi sasa ninavyoandika bado kinaingiza chaji.
Hii ni teknolojia ya hali ya juu sana kuipata kwa bei rahisi hivi, wireless charging. Nashauri makampuni mengine yawaige OKING kwa kutengeneza simu zenye feature nzuri kama hii kwa bei nafuu kabisa. Sisi watanzania wanyonge tutawaombea kwa Mungu awabariki. Kwa sasa sina hofu hata umeme ukikatika bado simu kiswaswadu changu hakitoisha chaji maana kinaendelea kujichaji hadi siku kitakapoharibika.
NB: Leo nimekimbia uwanja round 6 tu nikaanza kuhisi kifua kinabana na nashindwa kupumua na sio kawaida kwangu, mniombee.