Judithkaunda
Member
- Aug 21, 2022
- 90
- 231
Mnamo mwaka 1865, kwa mujibu wa vitabu vya historia. Biashara ya utumwa ilifikia tamati ulimwenguni kote. Mimi najua, na wewe unajua Afrika utumwa haukukomeshwa mwaka tajwa.
Ni mwaka 1961 Disemba uhuru wa Tanganyika ulitangazwa. Wewe unajua na mimi ninajua, nchi ipo huru lakini si kila mwananchi yupo huru. Maelfu wapo utumwani bado ikiwa ni zaidi ya miaka mia moja tangu biashara hiyo ilipowekewa katazo ulimwenguni.
Naitwa Judith, nilikaa utumwani kwa miaka sita. Na hii ni stori ya maisha yangu kwa ajili yako unayesoma.
Nikiwa ni binti niliyekuzwa katika maisha duni, ndoto yangu ilikuwa kuolewa na mwanaume mwenye kipato kikubwa. Mwanaume atakayenipa kila kitu ninachotamani katika maisha na kama Mungu akinijalia watoto nataka wasome shule za viwango vya juu, kiukweli niliuchukia umaskini, niliamini kama ntaolewa na tajiri basi nitapata kila kitu. Nilijidanganya sana na sikujua kama ninajidanganya.
Nilianguka katika masomo yangu, hili halikumshangaza mtu yeyote sembuse mimi. Wote tulitarajia. Huu haukuwa mwisho wa ndoto zangu za kuolewa na mtu mwenye kipato kikubwa.
Maisha duni, elimu iliyodorora. Bado nilifanikiwa kukibaini kipaji changu cha kupika chakula chenye ladha nzuri.
Nikiwa binti mdogo nilijichanganya kwenye sherehe na misiba ili mradi nipate nafasi ya kupika. Nilisifika sana pale kijijini, lakini uwezo wangu wa kupika sikuupa kipaumbele kabisa, na pale kijijini niliona pana nichelewesha kufanikiwa.
Nilikutana na mwenzi wa maisha yangu. Ndoto za kuolewa na tajiri zilikuwa zimeyeyuka tayari japokuwa sikuolewa na maskini kunuka kama mimi. Kwa shauku ya kuolewa sikuwahi kumweleza mwenza wangu juu ya kipaji changu cha kupika zaidi ya chakula cha nyumbani. Nilichagua kusubiri niizoee ndoa ndipo nimshawishi aweze kunipeleka shule ya mapishi. Lile lilikuwa kosa.
Niliolewa nikiwa na miaka 17 tu. Ile ndoa ambayo watu walipiga vigelegele pindi ninatia saini kwenye hati ya ndoa, sikujua na wao hawakujua kuwa ilikuwa ni hati ya kuingia utumwani.
Kwenye vitabu vya dini vinaeleza mwanamke amtii mumewe nae mume ampende mkewe. Maisha yangu yakaenda kinyume chake nikajitahidi sana kumtii lakini hakuonyesha mapenzi niliotamani kuyaona.
Hali duni ya maisha nilikotoka ikanitambulisha kama kijakazi kwenye nyumba ya mume wangu, mwanzo niliona ni sawa na kufurahia kuwepo mazingira yale. Ilimradi nipo katika ndoa.
Baada ya muda kupita hali ilibadilika ile ndoto ya kuwa na familia yenye furaha iliyeyuka baada ya kuona sithaminiwi kabisa.
Mume wangu alikuwa mkubwa kiumri akaniona kama mdogo wake wa mwisho anaeweza kumuamrisha afanye chochote na akamtii, nilitegemea nimwambie nini kuhusu familia.
Mtumwa hakuwahi kuruhusiwa walau kulijua jina la mtawala wake, alitakiwa kumuita bwana mkubwa. Mimi sikutakiwa walau kujua mume wangu anaongea nini katika simu, alizungumza lugha ya kigeni huku anacheka.
Hakuwahi kunipeleka walau ofisini kwake, sikujua lolote juu ya biashara zake. Niliishi kama roboti.
Ni mtoto wa mjini ntamwambia nini kuhusu mapenzi kila kitu anajua, hata nilipo jaribu kujiremba na kumuonyesha mapenzi niligeuka kituko na mshamba wa mapenzi. Basi jitihada zangu nyingi ziligonga mwamba nilichotakiwa ni kusikiliza amri yake, hakukuwa na mapenzi hata busu niliishia kuliona kwenye tamthilia, alinikumbatia wakati wa tendo na kuniamrisha nifanye anavyotaka. Hakujali muonekano wangu na kwanini nipendeze kwa ajili ya nani? wakati yeye alinipenda hivi nilivyo na kama angetaka kuoa mrembo asingeshindwa kwani wamemzunguka kila mahali.
Babu zetu katika maisha yao ya utumwa walitakiwa kufanya kazi wakati wote bila kuhoji. Naam! Nami nilikuwa mtu wa kushindia nyumbani, kuhakikisha kila kitu kinakuwa safi. Hakuwahi kuthubutu kuweka msaidizi wa kazi hata nilipozidiwa na ulezi wa watoto alionizalisha mfululizo.
Aliwaogopa viongozi wa kiroho akanipa siku moja pekee ya kujichanganya na watu siku ya ibada. Hakujali kuhusu ujirani, akanizuia kuwa na marafiki. Nilichokosa ni nila katika shingo yangu lakini nilikuwa mtumwa kamili.
Nilitumia vizuri karama yangu pale palipotokea tukio kanisani, nilisifika na baadhi walinialika sehemu zingine kupika lakini mume wangu alinizuia na kunifanya nikate tamaa kabisa.
Sikuacha kutafuta namna ya kumshawishi ingawa ilikuwa ngumu kufanya hivyo kwa sababu mahitaji yote huwa ananunua mwenyewe. Ninachotakiwa kufanya nikuandika orodha ya mahitaji yote muhimu na lisilo la lazima analifuta, ilikuwa ngumu sana kwani nilitakiwa niandike mpaka viberiti navyotumia kwa mwezi. Ilikuwa ngumu sana kupata pesa yake na hakutaka niitafute yangu. Alikuwa mkoloni mweusi!
Sikuchoka nikajipanga kumshawishi tena kuhusu biashara ya ndoto yangu, nikapika chakula kizuri kwa ufundi wangu wote nikiamini lazima akisifie, maskini mimi sijui kwanini sikufikilia kwa makini kile chakula kitawezaje kumshawishi mtu ambae mara nyingi hali chakula nyumbani, na hata akiwa ofisini anaagiza vyakula vya gharama kubwa mtandaoni analetewa. Alikula na hakusema chochote na niliogopa hata kumuuliza mara nyingi amekuwa mkali sana kwangu na hali hiyo ilinifanya nipoteze kujiamini kabisa.
Ujauzito wa tatu ulikuja na changamoto ya mwili kuchoka. Nikaambiwa ninajidekeza angali kijiji ninachotoka mwanamke hata akiwa na mimba ya miezi tisa anaenda kisimani kuchota maji na kufanya palizi mashambani.
Siku nilipoacha kufua nguo zake kwa sababu ya ubovu wa hali yangu. Alinipiga kama mtoto mdogo na majirani wakisikia naugulia.
Ile nyumba ya kifahari niliyokuwa naishi ilikuwa ni kambi ya utumwa. Ndoa ni pingu za maisha, ile yangu iliniunganisha mikono na miguu pamoja na akili yangu. Sikuwa huru.
Nilizitamani zile siku nilizokuwa kijijini kwetu nikisifiwa kwenye matukio baada ya watu kushiba, na vile vicheko vya familia yangu sebuleni wakila ugali na matembele alafu nikawaletea nyama iliyoungwa vizuri niliyotoa kwenye sherehe. Nilitamani kurudi nyumbani hatimaye.
Kifo cha mjomba wangu nilikipokea kwa uchungu lakini ikawa ni fursa ya kurejea nyumbani. Akilini mwangu nilipanga nikawaeleze wazazi wangu kila kitu na mateso yote nayopitia, kumbe nilikuwa najidanganya.
Siku ya safari ikawadia kama kawaida ya mume wangu aliwanunulia zawadi nyingi ndugu zangu. Tulipofika tulipokelewa kama ndiyo tulikuwa wahusika wakuu. Baada ya msiba mume wangu alianza kugawa zawadi zake na ghafla yale majonzi ya msiba yakageuka vicheko na furaha, nilisifiwa na kuonekana mwenye bahati ya mtende, hata mama yangu anayejua afya yangu nakuona ilivyo dhoofu aliona ni kwa sababu ya kunyonyesha mtoto na hakutaka kujua kama nina tatizo lingine.
Kabla ya siku ya kuondoka nilipanga kuwaeleza wazazi wangu yanayonisibu. Kweli nilipata nafasi ya kuongea na mama yangu mwenye huruma, lakini kilichonikuta nilijuta kwanini nilisema.
Niliwekwa kikao na familia nzima na mama hakuwa na mengi ya kusema zaidi alinukuu baadhi ya maneno yangu
"Jamani ndugu yenu katuita hapa kutwambia anataka kuachana na mumewe kwa madai ya kwamba mume wake hamuonyeshi mapenzi na hataki kumsapoti ndoto zake." Ndugu zangu wote walinijia juu na kunilaumu kwanini namsema vibaya shemeji yao, walinikumbusha mambo yote aliyowafanyia na kutakiwa kuwa na shukurani
Ni kweli nilikuwa mbinafsi, nilijifikiria mwenyewe na ndoto zangu, sikujali maamuzi yangu yatawaathiri vipi watoto wangu na ndugu zangu.
Hii kesi alishinda mume wangu bila hata kufikishwa kizimbani wala kutoa neno, kwani alikuwa na akiba ya mashahidi wakumtetea bahati mabaya mimi sikuwekeza katika hilo.
Nilimtazama dada yangu mkubwa aliyewahi kupewa mtaji na mume wangu akafungua saluni, na ndipo wanapata pesa ya kujikimu. Pembeni alikuwepo baba yangu anayesumbuliwa na uvimbe, mume wangu ndiye alimsafirisha na kwenda kutibiwa mjini na mpaka wakati huo kuna dawa anamuagizia kutoka mjini. Wadogo zangu wawili mmoja amepelekwa Veta kwa ajili ya masomo na mwingine yuko kidato cha nne ana ndoto za kusoma elimu ya juu na mume wangu kamuahidi kumsimamia.
Ntasema nini tena zaidi ya kuomba radhi na kuonekana nimechanganyikiwa. Narudi utumwani na sina tumaini lolote la kujinasua nimekubaliana na yote kuishi kwa ajili ya wengine.
Kosa moja la kimaamuzi la kusema ndiyo limegharimu maisha yangu yote nikashidwa kutimiza malengo yangu.
Na kusihi kama bado hujaingia kwenye ndoa tumia ujana wako vizuri huo ndio wakati wakujichanganya na watu unaotaka kuwa kama wao ni muda wa uhuru wa kwenda unapotaka wewe, huna majukumu ya lazima, olewa ukiwa umetosheleza maarifa na tayari unaishi ndoto zako. Na kama utaingia kwenye ndoa basi hakikisha mtu huyo yuko tayari kusapoti ndoto zako na kuelewa hisia zako. Usiingie huko kwa kuiga au tamaa za mwili, Usiingie huko kama huyo mtu hakusapoti, usiingie huko kwa kutimiza ndoto za wenzio.
Ndoa za wengine, magari ya wengine na starehe za wengine visikunyime raha na kukufanya ubadili vipaumbele na malengo yako, ila vikupe amasa tu.
Dada yenu nimeishi utumwani sitaki ndugu zangu muingie huko.
0682253906

Upvote
12