Nimeitwa kwa ajilli ya interview Lagos Nigeria CHEVRON COMPANY

Huyu lazima mwisho atalia kilio cha mbwa!mkuu kimbia wezi hao
 
haha hao lazima wakuambie utoe acc namba wakupe details zaidi hapo ujue imekula kwako
 
Kama hii ndiyo email ya kuitwa basi jitayarishe kuibiwa .Ushauri achana nao hao ni wezi na hii ni Scam,Period!
 
Unaweza kukuta mdau kasahawatumia mihela kibao ya kuprocess 'work permit'.
 
Huko ndo kutapeliwa kaka Assistant Accountant atoke TZ wakati uko Naija wako kibao!
 
nakwambia nina 100% sure hawa ni matapeli ya formation ya hiyo barua ni sawa kabisa na barua niliyowahi tumiwa mimi na nazozidi kutumiwa ila uwa sizijibu.
Jamani msikurupukie vitu amabvyo unatumiwa email sijui umepata kazi au umeshinda promotion wakati hukuwahi omba kazi wala shiriki kucheza.
 
Yeah na jana walikua na mkutano wa all permanent staffs!

Yeah,
@ Southrn Sun Hotel.
I was there for almost 4Years till May this year, but from acquirer side, not acquired.
Wamjua nani pale?
 
Mim niliapply kama refinery process operator,wameniita Lagos kwa interview...nilipe gharama za kwenda ambazo ntarudishiwa nikifika huko...na wamesema niende ubaloz wao hapa kwa ajil ya ku process vinavyohitajika.
 
ki english chenyewe hovyo hovyo tu inatosha kuonyesha kuwa matapeli wenyewe wala hawako smart,check hizo red, email za hotmail.com za mwaka 47 leo hii kampuni muhimuya wanasheria kama hii inatumia email adress za mtindo huu, wewe cheza nao kwa kuwatapeli na wewe kujifanya una interest uwafahamu vizuri ujuha wao, watanyamaza wenyewe.
 
Last edited by a moderator:
Yeah,
@ Southrn Sun Hotel.
I was there for almost 4Years till May this year, but from acquirer side, not acquired.
Wamjua nani pale?

ha ha we Shakir nahisi nakujua kabisa..ulikua upande wa chevron ama engen kabisa?
 
Last edited by a moderator:
Usiende dogo ni matapeli hao. hizo barua zimetumwa kwa watu wengi ni usanii mtupu!!!
waliwahi kupost nafasi zao JF so kama ulituma cv yako ndo maana wakakutumia hiyo invitation letter
 
hiyo ni dongo la macho kaka maana kuna jamaa yangu alitumiwa email last month aende Nov 5 kwenye interview lakini baada ya kufanya contact na Chevron wenyewe wakakataa hawajawahi kumtumia email. Kuwa makini NIgeria kuna wahuni wengi
 
Ndugu yangu,


Logically, kuna maswali mengi zaidi kuliko majibu. Je uliapply hiyo kazi? Kama siyo, wanakuita bila kuapply kwani ni wajomba zako? Je hata kama uliapply, moja ya sifa ilikuwa wanataka mtu kutoka TZ ? Maana ninavyoelewa Nigeria wana wasomi wengi na ajira ni tatizo na ukizingatia hiyo kazi ya uhasibu siyo siyo kivile hadi wamhitaji kutoka nje ya nchi.

Wakati mwingine jitaidi kusimama kwa miguu yako.
 
Itafika hatua tenda za west n north africa mtu haendi,hata kama ni kweli kwa utapeli wao
 
Usiende dogo ni matapeli hao. hizo barua zimetumwa kwa watu wengi ni usanii mtupu!!!
waliwahi kupost nafasi zao JF so kama ulituma cv yako ndo maana wakakutumia hiyo invitation letter

asante sana kwa ushauri.keep in touch.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…