Nimejiajiri kama Blogger, hata nawe unaweza jaribu

Nimejiajiri kama Blogger, hata nawe unaweza jaribu

Mjasiriamali M

Senior Member
Joined
Jan 15, 2013
Posts
142
Reaction score
69
Habari ndugu zangu, leo naomba nami niongee neno katika uwanja huu wa kijasiriamali, Mimi ni mhitimu wa Degree ya Uhasibu miaka 3 iliyopita, tangu kipindi hicho chote sijapata ajira ya kudumu na rasmi, Namshukuru Mungu niliwahi kusomea mambo ya I.T kwa level ya Certificate nilivyomaliza Form 6 mwaka 2007, sasa baasi, baada ya kusota miaka yote huku nikihangaika kwa hili na lile, nikapata wazo la kuwa Blogger, ingawa mwanzoni ilikuwa ngumu lakini sikuacha kujituma na kujifunza toka kwa waliofanikiwa kwani hata wao walianzia chini

. Kwa muda wa miezi sita ya mwanzo nilikosa Direction nzuri kwani kila kitu nilikuwa nataka kufanya au kuandika mimi, kuna kipindi nilikata tamaa na kuona kwamba Kupata mafanikio kupitia Blogging si kwangu mimi, hata hivyo kipindi hicho kigumu kilipita na nikapata kibarua fulani ambacho kilinifanya nijitume na kujikusanya katika suala zima la fedha na kuweza kununua laptop mpya na universal modem ambavyo ndio kama JEMBE na SHOKA langu.

Baada ya hapo nilijipanga kwa kuwa naandika Articles zenye kuvuta hisia za wasomaji wangu huku nikiendelea kujifunza nami kadri siku zinavyoenda. Kwa uchache nawashauri Vijana wenzangu ambao tuna access na internet na tuna muda kujifunza na kufanya hivyo kwani mimi nimeanza kuyaonja matunda ya blogging kupitia Google Adsense kwani hata leo nimetoka kuchukua Hela zangu Kupitia Western Union. Pia binafsi nimeanzisha blog ambayo tutakuwa tunaelekezana na kufundishana mambo mbali mbali ikiwemo na mbinu za kufanya ili kufikia mbali katika blogging.

Kwa vile si mtaalamu sana wa ki teknolojia na computer science ntakuwa natoa facts ambazo hata mimi mhasibu nilizipitia na mpaka leo nami napata kidogo kupitia Google Adsense.

Email: tzbloggers@gmail.com
 
Endelea kutiririka, unapataje mgao na ili upate pesa nyingi unatakiwa kufanya nini?
 
Asante kaka, first step ni kujitoa kwa hali na mali, na kikubwa ni muda wako kwa kuifanya hobby au mtazamo wako juu ya kitu fulani kuwa vivid kupitia blog yako, japo kuna mengi ya kujifunza mfano, blog yako itazungumzia nini, wakina nani wanafanya blogging kama wewe, tawira ya blog yako, vipi utakuwa unapost na direction kwa ujumla, pia ikumbukwe kuwa " making money online is as tough as making money offline" hivyo basi kujitoa na kujifunza kunahitajika sana.
 
Kikubwa zaidi ni Traffic(yaani idadi ya watu wanaotembelea blog yako na page views kwa siku) mfano ikiwa blog yako inapata unique visitors 100 kwa siku na page views angalau 1500 kwa siku basi unakuwa katika position ya kupata euro 2-5 kwa siku. Pia hakikisha content zako ni za ukweli na hau violate terms and conditions za u publisher.
 
Safi sana mkuu..hivi ndio vitu tunataka kuona vijana wa kizazi hiki wanakuja navyo..

Nimeipenda sana hii idea yako, big up sana
 
Asanteni wakuu, hili ni letu soote. kwa Nigeria wameshtuka mapema na kuna bloggers wengi wanafanya vizuri kuliko hata watu weupe.
 
Back
Top Bottom