Captain mopao
Senior Member
- Feb 25, 2021
- 133
- 384
Habari zenu wadau
Mimi ni mfanyabiashara wa jeans za mtumba za kiume, sina muda sana kwenye hii biashara ni kama miezi kadhaa.
Sehemu zangu ni katika minada na magulio katika kuzunguka kwangu nikakutana na jamaa yeye anauza urembo nae pia tunazunguka wote katika minada.
Biashara yake ilianza kunivutia kwa jins alivo na wateja, maana tukifika tutafungua wote biashara lakini yeye ni wa kwanza kupata wateja na kina dada hawakauki katika biashara yake.
Taratibu nikaanza kumdodosa kuhusu biashara yake na jamaa bila hiyana akanipa feed back zote.
Nilichogundua ingawa yeye ana wateja wengi kuliko mimi namzidi mauzo maana mimi nahitaji wateja wawili kuifikisha alfu kumi ila yeye anahitaji wateja kumi au zaidi kufikisha alfu kumi.
Mfano yeye anauza heleni mia 3 au kitana mia 5 au lesso alfu moja.
Wakati mimi nauza kila suruali moja nauza alfu tano,
Nilianza kudata na biashara ambayo ingekuja kunishinda so nimejifunza kutokufata mkumbo.
Siku njema wadau.