Nimejikuta ninakichukia chama changu

Nimejikuta ninakichukia chama changu

Mtetezi.com

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
3,134
Reaction score
3,584
Mimi ni kada wa chama cha mapinduzi kwa zaidi ya miaka 18 sasa lakini kwa yanayoendelea sasa nimejikuta kukichukia sana chama changu.

Yanayonikera
1. Ukosefu wa ajira
2. Hali mbaya ya kiuchumi
3. Ufisadi
4. Utekaji wa wakosoaji ambao pia wengine ni ndg, jamaa na marafiki zetu
5. Vyombo vya ulinzi na usalama kutumika kisiasa
6. Bunge la hovyo kupita kipindi chochote huko nyuma

Ninafahamu itawafikia wakuu.

Tafadhali hii nchi ni yetu sote hebu tuishini kwa kuvumiliana, kuheshimiana na kuhurumiana.

Sio tu kwamba mnawachosha wapinzani hata sisi wanachama wenu mnatukera mno hamjui tu.
Sasa jiulize kama mtu mwenye level ya kada anakereka namna hii mtu asiye na chama itakuwaje

Hayo mnayoyafanya hamjengi bali mnabomoa.
Mana hii chuki mnayoitengeneza ni bomu litakalokuja kulipuka

Nimesikia siku hizi ukisema unanyamazishwa sasa sisi wanachama wenu mtamuongoza nani?

Nimetema nyongo
Ninaamini kila mtu atakufa siku yake ikifika hivyo waacheni watu wakosoe.
 
Back
Top Bottom