Nimejiuliza sana hili swali kuhusiana na Jf

Nimejiuliza sana hili swali kuhusiana na Jf

MJUMBE WA AMANI

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2016
Posts
262
Reaction score
238
Members wengine wana shirikije hapa Jamiiforums?

Hili swali limenishangaza sana pale nilipoona kuna members 350k but ukiangalia washiriki ni wale wale.
Kuna majukwaa utaona waanzisha mada ni wale wale, sehemu nyingine robo page ni mada za mtu mmoja.Hivi ni kweli kwamba wahusika wengine hawana cha kutushirikisha.

Pili na muhimu, hivi member wa jf akiaga dunia huwa inajulikana.Najua kuna baadhi ya watu wanafahamiana ila tukio kama hilo likitokea taarifa zinaletwaga kwa wahusika waliosalia?
We are living in the technology and information era, so guys let us live the era.

Ni hayo tu wadau.
 
Ni kweli kuwa mara nyingi members wanaojulikana ni walewale na ndio hasa huleta mada/threads za kujadili, ila jua tu kuwa kuna members wengine walishajiunga kupata habari za masuala mbalimbali but they are not active members, they only intend to acquire informations from this forum.
 
Akifa hutomuona akichangia humu
 
Mjumbe wa amani bhana, wewe mwenyewe una siku 21tu tangu uanze kuchangia hapa jukwaani.
 
Ni kweli kuwa mara nyingi members wanaojulikana ni walewale na ndio hasa huleta mada/threads za kujadili, ila jua tu kuwa kuna members wengine walishajiunga kupata habari za masuala mbalimbali but they are not active members, they only intend to acquire informations from this forum.
Heh! kwahiyo hao wa hivyo wanakuja kupakua news na kutimua...wahawana cha kushirikisha?
 
Mjumbe wa amani bhana, wewe mwenyewe una siku 21tu tangu uanze kuchangia hapa jukwaani.
Mkuu tatizo siyo muda wa kujiunga,shida ni pale unakuta ID ya 2012 lakini imepost mara 20 tu.Hujawahi kuona hiyo?
 
Instagram Ipo Hivi

Unafollowers 10k ila unapata like 200 comment Moja.. Followers wengine Washapoteza simu.. wamefariki... Au wapo ila hawatumii tena

Hii pia Ina reflect JF
 
Heh! kwahiyo hao wa hivyo wanakuja kupakua news na kutimua...wahawana cha kushirikisha?
certainly!!! they term jf as their source of news, hawataki kuchangia wala kupost chochote, wanakuja kuchota taarifa na kusepa, tena ukute wanafaham majina ya wachangiaji maarufu hapa jf.
 
Instagram Ipo Hivi

Unafollowers 10k ila unapata like 200 comment Moja.. Followers wengine Washapoteza simu.. wamefariki... Au wapo ila hawatumii tena

Hii pia Ina reflect JF
Ha ha ha, sure that's it. Utamkuta Celeb ana followers 200k ila ana like 2000, ila jf ni tofauti na 'Gram mkuu.
 
Wapo sana tu. Jukwaa kama la siasa imekuwa sehemu ya propaganda, vile viID unavyoviona mara kwa mara ni taasisi za propaganda hivyo wanashindana kupost na kuchafuana.
 
kuna wengine kazi yao kusoma tu mada ila hawachangii chochote ndio maana ukianzisha uzi utakuta unaviewer 2000 walioreply 20
Kweli mkuu tena mara kibao sana, ila viewers si pamoja na wale guest au?
 
Ndio hapo nikauliza je wale 350k ni kweli wapo hai? Kama mtu hai hachangii atatofautishwa vipi na mtu aliyeaga?
Wapo waliofariki, wapo waliosahau code za account na pia wapo waliostaaf maana umri hauruhu kuendelea kuchangia humu. Hata ugumu wa maisha umewafanya watu walekeze jf
 
Wapo sana tu. Jukwaa kama la siasa imekuwa sehemu ya propaganda, vile viID unavyoviona mara kwa mara ni taasisi za propaganda hivyo wanashindana kupost na kuchafuana.
Tobah! yaani ID moja inaweza kuwa na watumiaji zaidi ya mmoja? Kweli siasa ni maji taka.
 
Wapo waliofariki, wapo waliosahau code za account na pia wapo waliostaaf maana umri hauruhu kuendelea kuchangia humu. Hata ugumu wa maisha umewafanya watu walekeze jf
Ha ha ha, mbavu zangu mie.
 
Back
Top Bottom