Mie nakupa Moyo, hakuna kitu ambacho hakiwezekani pale utakapomtanguliza Muumba ( Mungu wa Ibrahim, Isaac na Yacob), mshukuru kama umefanikiwa kuwa na huo mtaji. Sio haba, Napenda zaana kusoma taarifa za wafanyabishara maarufu na ma CEO wa makampuni makubwa, wengi walianza walianza ni miraji midogo kabisa na ma CEO wengi walikuwa wafanyakazi wakawaida<br />
<br />
Cha msingi,kama umehamua kufanya hiyo shughuli, Ipende, jitume, jifunze na omba ushauri kwa watu wanaofanya hiyo biashara. Unaweza hata kutumia internet kujifunza zaidi kuhusu dhahabu, hususani utambuzi, Kipindi cha sabasaba au nanenane jitahidi kutembelea wakama wa serekali wa madini. wapo wataalau ongea nao, ikiwezekana jenga mazoea nao watakupa msaada mkubwa tu.Baada ya muda utajenga uwezo mabank yatakuamini na unaweza ukakopa kuongezea mtaji wako. naamini with time na wewe utakuwa mfanyabiahsara mkubwa wa dhahabu kama wa- lebanon, waarabu, wachina, wanaotoka kwao na kwenda moja kwa moja kwa wachimbaji wadogo na kuchukua kwa bei chee na kwenda kuuza kwa bei kubwa. Mwaka juzi nilikuwa shinyanga vijijini nikakutana na wahindi, wachina wanatafuta diamond kwa wachimbaji wadogo wadogo, nilijiuliza kungekuwa na watanganyika wanaoyanunua hayo madini huko maporini na kwenda kuwauzia hao wachina, wahindi na waarabu kwenye miji yetu mikubwa kama arusha na DSM si angalau mzinguko wa pesa ungekuwa mpana na kuwafaidisha watanganyika wengi<br />
<br />
Usikate tamaa kwa kuwa ushahamua kuifanya hiyo bishara ni vema ukaanza sasa na usisubiri kesho. Naamini with time lazima utayafikia malengo yako ya maisha