Nimekata tamaa ya kupona .

Joined
Mar 8, 2014
Posts
60
Reaction score
11
Habari wa jukwaa letu la JF doctors?

Jamani nimekata tamaa ya kupona macho, nimetembea kwenye hospital nyingi tu naambiwa hawaoni tatizo wananipa tu ushauri wa kula vyakula na matunda na pia kutumia miwani ili kurekebisha uono hafifu, hii ina maana kuwa hospital hakuna tiba ya macho zaidi ya kupewa miwani tu.

Mimi binafsi sipendi kutumia miwani bali ni kupona kabisa tatizo la macho, niliwahi kuambiwa nimechezewa lakini hata tiba za jadi hazijanisaidia zaidi ya kufuja pesa. naombeni ushauri wadau nifanyeje?
 
Halafu nauliza kuhusu tiba mbadala, wapo baadhi ya madaktari wamenambia kuwa hospital hazina dawa za matatizo ya macho zaidi ya operation, hivyo naambiwa niende kwa wataalam wa tiba asilia wanaotibu kwa vidonge, pia wapo wanaoniambia kuwa kama hospital hawana dawa ya kunitibu, basi! hata tiba za asili za kina dr. ndodi hazitanisaidia, hivyo nakata tamaa ya kupona kwa kuwa hospital hakuna tiba ya tatizo langu.

Ni dr.gani anaweza kunipatia tiba kamili kwa huko dar? mimi nipo dodoma.
 
Njoo muhimbili kitengo cha macho upate msaada, ili hata kama hutapona kabisa tatizo lako basi wataalamu wakusaidie kulielewa vyema na kwa undani ili roho yako angalau itulie.
 
njoo muhimbili kitengo cha macho upate msaada, ili hata kama hutapona kabisa tatizo lako basi wataalamu wakusaidie kulielewa vyema na kwa undani ili roho yako angalau itulie

Mkuu kama ccbrt wameshindwa hapo muhimbili wataweza kweli?
 
Umechezewa macho? Kwa faida gani? Si bira wangekuchezea sehemu za siri wakapata walau raha kidogo?

Mbona unaleta utani kwenye mambo nyeti hivi rafiki yangu? Alafu umejua mleta mada ni jinsia gani
 
Vaa tu miwani hakuna jinsi matatizo mengine ya macho ni ya kurithi,mimi nina tatizo la kutokuona mbali miaka kumi sasa navaa miwani, madaktari hawashauri kufanyiwa operation na ujana utaharibu macho,operation ni kwa wazee wasioona sana.
 
Watu wengine jmn!!kams huna cha kusema kaa kimya haikugharimu.acha wenye ushauri wakumsaidia waje.daah!!kifupi umechosha mdau.
 
hivi uumwe macho kiukwelikweli na unaambiwa uvae miwani utakataaje? mbona watu wanavaa miwani na maisha yanasonga mbele!?na ujue cku zinavyozidi kusonga ndo yanazidi kuharibika!
 
Reactions: BAK
Kama hutaki kuvaa miwani basi waambie Madokta wayang'oe hayo macho, utapona hilo tatizo linaokusumbua...
 
hivi uumwe macho kiukwelikweli na unaambiwa uvae miwani utakataaje? mbona watu wanavaa miwani na maisha yanasonga mbele!?na ujue cku zinavyozidi kusonga ndo yanazidi kuharibika!

Huyu Chalii hayuko siriaz Bana...
 
Mkuu acha imani potofu wakuchezee macho ili iweje wakati umejiexpose kwenye region ambayo kuumwa macho ni kawaida sana(Dodoma)! Ulizani wale wagogo ombaomba huku mijini wamejitia minyaa eee!? Fuata ushauri wa daktari mkuu kugomea miwani unajikomoa mwenyewe!
 
Tatizo lisikie kwa mwenzio lakini siku likiwa kwako,
utalia na kusaga meno.

Pole sana; angalia usiweke madawa kwenye macho
unaweza ukayaharibu kabisa;

God be with you.
 
Hakuna nyeti kuliko nyeti zenyewe. Kaambiwa miwani hataki, anasema kachezewa, kuna raha gani kuchezea macho ya mtu?

Mbona unaleta utani kwenye mambo nyeti hivi rafiki yangu? Alafu umejua mleta mada ni jinsia gani
 

Mkuu njoo nikupeleke kwenye maombi uombewe,kama una amimi na una nia nijulishe nikuagize sehemu ya maombi hakika utapona,lisilowezekana kwa binadamu,kwa Mungu lawezekana
 
ccbrt walikwambia tatizo hasa ni lipi? na je wewe unalielewa?

Kuna wazungu pale ccbrt waliniambia tu niwe nakula mbogamboga tu, hii ina maana kwamba nitakuwa na upungufu wa vitamini C kwani baada ya hapo nilishauriwa nitumie miwani tu kwamba kadiri siku zinavyokwenda itakuwa inanisaidia na hatimaye kuacha kabisa kuitumia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…