Nimekatwa Shillingi 70,000 na Vodacom

Nimekatwa Shillingi 70,000 na Vodacom

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Jana nilikuwa sehemu nikawa nina mahitaji ya haraka ya pesa. Huwa sina tabia ya kujikopesha maana naonaga ni kuingia gharama kusiko kwa lazima ila sikuwa na jinsi.

Sasa nikasema nijikopeshe shilingi 370,000 kupitia MPAWA, Vodacom wakakata 70,000 juu kwa juu. Nimewapigia wanasema ndiyo makato yao hayo 19%.

Huu uhuni utaisha lini? Unakata makato hayo kwa hela unayotaka urudishiwe ndani ya mwezi mmoja?
 
Vodacom wanakata makato makubwa sana kila kona,usiombe ulipe kwa simu kutoka mtandao mwengine kuja voda
 
Back
Top Bottom